Mtuhumiwa wa mauaji ya Rwanda, Jean Claude Seyoboka, wakati alipowasili KIgali.
Afisa wa
zamani kwenye jeshi la Rwanda, amewasili jijini Kigali baada ya
kusafirishwa kutokea nchini Canada, akituhumiwa kuwa alihusika kwenye
mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambayo watu laki 8 waliuawa.
Mwendesha
mashtaka wa Rwanda, Jean-Bosco Mutangana, amethibitishwa kurejeshwa
nchini humo kwa mtuhumiwa Jean Claude Seyoboka, usiku wa kuamkia leo,
ambapo sasa atajibu tuhuma za mashataka ya mauaji yanayomkabili.
Seyoboka,
ambaye alikuwa ni Luteni wa pili kwenye jeshi la Rwanda, anatuhumiwa
kuhusika na mauajiya watusi zaidi ya 72 jijini Kigali na pia anadaiwa
kuwa alihudhuria vikao vilivyoidhinisha mauaji hao.Machafuko hayo
yaliyodumu kwa miezi minne, ambapo watu zaidi ya laki 8 waliuawa wengi
wakiwa watusi, yalichangiwa baada ya kudunguliwa kwa ndege iliyokuwa
imembeba rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana ambaye alikuwa Muhutu,
mwezi April mwaka 94.
Seyoboka
aliwasili nchini Canada mwaka 1995, ambako alipatiwa hifadhi ya kudumu
nchini humo mwaka mmoja baadae.Hata hivyo kibali cha hifadhi yake
kilitenguliwa miaka kumi baadae, baada ya kutolewa ushahudi kwenye
mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda iliyokuwa jijini
Arusha, Tanzania na kumuhusisha na mauaji hayo.
Mamlaka
nchini Rwanda zilitoa waranti ya kukamatwa kwa Seyoboka mwaka huu,
lakini alipigana kupinga kurejeshwa nchini mwake kwa kile alichosema
anahofia usalama wake na mateso.
Seyoboka
anakuwa mtuhumiwa wa pili wa mauaji ya kimbari kusafirishwa kutoka
nchini Canada, baada ya mwanasiasa wa zamani wa nchi hiyo Leon Mugesera
kurudishwa nchini Rwanda mwaka 2012.
Mugesera
alihukumiwa kifungo cha maisha jela, mwezi April mwaka 1994 kwa madai
ya kuhusika kwenye mauaji ya maelfu ya raia.Juma lililopita pia,
mwendesha mashtaka wa Uholanzi, alithibitisha kuwa raia wawili wa Rwanda
ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo, nao watarejeshwa nchini mwao.
Nchi
ya Rwanda iliomba kurejeshwa nchini humo kwa raia wake Jean-Claude
Lyamuremye na Jean-Baptiste Mugimba, mwaka 2012 na 2013, ili warudi
kukabiliana na tuhuma za kesi za mauaji na uhalifu dhidi ya binadamu
0 comments:
Post a Comment