Mwanafunzi
wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Gerezani, Shakil Sures
amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya
kujeruhiwa kwa risasi na polisi kwenye mazingira ya kutatanisha.
Tukio
hilo lililotokea Jumatatu eneo la Fire, Upanga licha ya watu kusikia
milio ya risasi, kushuhudia polisi wakipita na kumuona kijana huyo akiwa
tayari kajeruhiwa, lakini hakuna mwenye maelezo sahihi kuhusu nini
kilitokea hadi askari hao wakachukua hatua hiyo.
Baadhi
ya waliokuwapo eneo la tukio siku hiyo walidai kuwaona askari waliokuwa
eneo hilo wakirusha risasi, bila kujua walikuwa wakipambana na nani.
Mmoja wa mashuhuda, Athumani Simba alidai walidhani ni majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi, baada ya kuona gari la polisi likipita eneo hilo.
Mmoja wa mashuhuda, Athumani Simba alidai walidhani ni majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi, baada ya kuona gari la polisi likipita eneo hilo.
“Niliwaona
askari wawili wakielekea eneo la Fire huku wakipiga risasi, ghafla
nilimuona mwanafunzi akilia huku akiwa ameshika mguu wake akiomba
msaada,” alisema Simba.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo jioni ya Jumatatu na kwamba jeraha lake linaendelea vizuri.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo jioni ya Jumatatu na kwamba jeraha lake linaendelea vizuri.
“Tumempokea mwanafunzi Shakil juzi jioni na kidonda chake kimesafishwa na kinaendelea vizuri,” alisema Aligaesha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Hamduni Salum alisema upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea. Hata hivyo, hakueleza mazingira ya tukio lenyewe yalivyokuwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Hamduni Salum alisema upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea. Hata hivyo, hakueleza mazingira ya tukio lenyewe yalivyokuwa.
“Tunawashikilia
askari polisi wawili waliokuwa zamu siku hiyo ya tukio, upelelezi
unaendelea ili kuangalia kwa nini walitumia nguvu kubwa kiasi hicho,” alisema Kamanda Salum.
0 comments:
Post a Comment