Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua
jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete ambapo
aliwataka walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao na
kutafuta nyumba mbadala ili kuwezesha zoezi la ujenzi wa barabara kuanza
na zoezi la fidia lifuate baadaye.
Mbunge wa
Makete Profesa, Norman Sigala akifafanua jambo kwa wananchi wa Jimbo
hilo kuhusu umuhimu wa kutafuta nyumba mbadala ili kupisha ujenzi wa
barabara ya Njombe –Makete KM 109 utakaoanza hivi karibuni.
Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akimshukuru Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kufuatia hatua ya
ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Njombe na Ruvuma.
Wanananchi
wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Hayupo pichani).
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka
wananchi waliowekewa alama za kubomoa nyumba zao zilizopo pembezoni mwa
barabara ya Njombe-Makete hadi Mbeya KM 205 waanze kuhama kwenye nyumba
hizo ili kupisha zoezi la ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Akizungumza
mara baada ya kukagua barabara hiyo Eng. Ngonyani amesema awamu ya
kwanza ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya
kupatikana mkandarasi na mkandarasi mshauri ambayo itahusisha sehemu ya
Njombe hadi Makete KM 109.4.
“Kuweni
waadilifu waliowekewa alama za kijani kwenye nyumba zao watalipwa fidia
lakini wenye alama nyekundu hawatalipwa hivyo ni vizuri wote kutafuta
maeneo mengine ya makazi ili kuepuka usumbufu mara zoezi la ujenzi
litakapoanza”. Amesema Eng. Ngonyani.
Eng.
Ngonyani amesema kwa kuwa kazi ya ujenzi na ulipaji fidia zinagharamiwa
na Serikali ni vema zoezi la ujenzi wa barabara likaanza wakati Serikali
ikitafuta fedha kwa ajili ya fidia.
“Ili
tuweze kufanikiwa katika mambo yote tumeona tuanze na zoezi lenye
gharama kubwa ambalo ni ujenzi wa barabara kisha zoezi la fidia
litaendelea wakati ujenzi wa barabara unaendelea”. amesisitiza Eng.
Ngonyani.
Naye Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali kwa jitihada
za ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma
na ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuweka lami barabara inayokwenda
kwenye hospitali ya Mkoa wa Njombe na ile inayoenda hospitali ya
misheni ya Ikonda wilayani Makete ili kuwezesha barabara hizo kupitika
kwa urahisi wakati wote wa mwaka.
Katika
hatua nyingine Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigara amemuomba Naibu
Waziri Eng. Ngonyani kuhakikisha Mkandarasi anayejenga barabara ya
Njombe –Makete na Makete –Mbeya kupitia Kitulo anaanza kazi iyo kwa
wakati ili kuongeza kasi ya wananchi kubomoa nyumba zao katika maeneo ya
hifadhi ya barabara na hivyo kuunganisha kirahisi mkoa wa Njombe na
Mbeya kwa barabara ya lami.
Naibu
Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya Barabara,
Bandari na Mawasiliano katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambapo
tayari amekamilisha ziara yake katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Ruvuma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment