Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknlojia Imewataka wanafunzi wa St. Joseph
walioamishiwa katika chuo kikuu cha Dodoma kurudia mwaka kwa kile
kilichobainika kuwa na ujuzi na maarifa usiokidhi viwango vya chuo cha
Dodoma.
Wizara hiyo pia imesema kwamba watakaogomea uamuzi huo watatakiwa kurudi makwao .
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako alisema, ni lazima wanafunzi hao warudie mwaka
kwani wamepimwa na kubainika kuwa na uwezo mdogo hivyo hatua ya kuwataka
kurudia mwaka ni nafasi ya pili kwao.
Prof.
Ndalichako alisema, kwa sasa wizara yake inaandaa ripoti ya vyuo
vinavyofundisha chini ya viwango ambapo amesema mara tu baada ya
kukamilika ripoti hiyo, itatolewa na kwamba kwa wale wanafunzi ambao
vyuo vyao vimefungwa kwa kutokidhi vigezo ni lazima wapimwe kiubora ili
kupata wanafunzi watakao kidhi vigezo vya soko la ajira.
Aidha,
Prof. Ndalichako ametoa onyo kwa wanafunzi ambao wamegushi nyaraka
mbalimbali ikiwemo za vifo vya wazazi wao ama ugonjwa na kufanikiwa
kupata mkopo wa elimu ya juu kwa njia ya udanganyifu kuwa wizara hiyo
inafanya uhakiki na pindi watakapo bainika hatua kali zitachukuliwa
dhidi yao.
0 comments:
Post a Comment