- MTU MMOJA AMEUAWA NA WATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WILAYANI NYAMAGANA.
- MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA VITENDO VYA UKATILI MJUKUU WAKE WILAYANI NYAMAGANA.
- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLSI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA DARASA LA TATU WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA
TAREHE 17.11.2016 MAJIRA YA SAA 20:30HRS KATIKA MTAA WA NKURUMA KATA NA
WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMKE MWENYE
ASILI YA KIASIA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA VASANTBEN RAMANBHAI, MIAKA 48,
MUHINDI, MAMA WA NYUMBANI NA MKAZI WA MTAA WA RUFIJI, ALIUAWA KWA
KUPIGWA RISASI MOJA SEHEMU YA MGONGONI NA WATU WANAOZANIWA KUWA NI
MAJAMBAZI WALIVAMIA DUKA LA MIAMALA YA FEDHA YA M –PESA, TIGO PESA NA
AIRTEL MONEY NA BIDHAA NYINGINE MBALIMBALI MALI YA LAURENT PETER NA
KUFANIKIWA KUPORA FEDHA NA SIMU TANO.
INADAIWA
KUWA MAREHEMU ALIKWENDA DUKANI HAPO KUPATIWA HUDUMA, NDIPO GHAFLA
WALITOKEA MAJAMBAZI WATATU WAKIWA NA PIKIPIKI MMOJA KATI YAO AKIWA
SILAHA NA KUFYATUA RISASI KADHAA HEWANI, NDIPO RISASI MOJA ILIMPATA
MAREHEMU SEHEMU YA MGONGONI NA KUFARIKI DUNIA . AIDHA KATIKA TUKIO HILO
MAJAMBAZI HAO WALIFANIKIWA KUPORA FEDHA AMBAZO HAIJAFAHAMIKA NI KIASI
GANI HADI SASA NA SIMU TAN0, SIMU TATU KATI YA HIZO ZILIKUWA ZIKITUMIKA
KUFANYA KAZI YA KUTUMA MIAMALA YA FEDHA NA NYINGINE MBILI ZIKITUMIKA
KATIKA MAWASILIANO YA KAWAIDA, ZOTE MALI ZA MWENYE DUKA.
JESHI LA
POLISI LIPO KATIKA UPELELZI NA MSAKO WA KUHAKIKISHA WATU HAO
WANAKAMTWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA
UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO
SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTULIA
NA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KATIKA KUFANIKISHA
KUWAKAMATA WATU HAWA WENYE NIA OVU DHIDI YA USALAMA WA WANANCHI NA MALI
ZAO. TUNAENDELEA KUWASIHI WANANCHI WATULIE WASIWE NA MASHAKA JESHI LAO
LA POLISI LIPO VIZURI KUHAKIKISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO
UNAIMARISHWA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MNAMO
TAREHE 11.11.2016 MAJIRA YA 20:00HRS KATIKA MTAA WA MAHINA KATA YA
BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA
ALIYEJULIKANA KWA JINA LA AMINA HAMISI MIAKA 56 MKAZI WA MAHINA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUMLAZIMISHA KULA KINYESI
MJUKUU WAKE AITWAYE REHEMA SADIKI MIAKA 07, KITENDO AMBACHO NI UKATILI
DHIDI YA MTOTO NA NI KOSA KISHERIA.
INADAIWA
KUWA SIKU TAJWA HAPO JUU MTOTO HUYO ALIKWENDA CHOONI KUJISADIA NA
KUSHINDWA KUMWAGIA MAJI ILI KUONDOA KINYESI CHAKE , NDIPO BIBI YAKE ILI
KUMUADHIBU ALIMUAMURU KULA KINYESI HICHO, KITENDO AMBACHO MTOTO HUYO
ALIKITEKELEZA.
AIDHA
BAADA MTUHUMIWA KUFANYA UKATILI HUO KWA MTOTO. RAIA WEMA WALITOA
TAARIFA POLISI AMBAO WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA
MTUHUMIWA HUYO. UPELELEZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI
MARA MOJA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO
SENGA ANATO WITO KWA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA AKIWATAKA KUSHIRIKIANA KWA
PAMOJA NA JESHI LA POLISI KATIKA KUDHIBITI VITENDO VYA UKATILI HASA KWA
WATOTO KATIKA MKOA WETU. ALIONGEZA KUWA UKATILI NI KOSA KISHERIA HIVYO
WANANCHI WAACHE KUFANYA VITENDO HIVYO NA WATAKAO BAINIKA SHERIA
ITACHUKUA MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU.
KWAMBA
TAREHE 16.11.2016 MAJIRA YA SAA 19:00HRS KATIKA MTAA WA NYABUROGOYA KATA
YA NYEGEZI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTOTO JINA
TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 11, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU
SHULE YA MSINGI NYABUROGOYA ALIBAKWA NA MTU ALIYEJULIKANA KWA JINA LA
JAMES CHIRAGWIRE MIAKA 42, AFISA MTENDAJI KATA YA MKUYUNI NA
KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI KATIKA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, KITENDO AMBACHO
NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA
KUWA MTUHUMIWA ANAISHI JIRANI NA NYUMBANI KWA MTOTO HUYO ANAYEISHI NA
MAMA YAKE MZAZI, AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA NA MAZOEA YA
KUMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUINGIA NAE NDANI KWAKE NA KUMPATIA FEDHA NA
ZAWADI NDOGONDOGO NDIPO SIKU HIYO ALIPOFIKA NYUMBANI KWAO, MTOTO
ALIMKUTA PEKE YAKE NDIPO ALIMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUMFUNGA KITAMBAA
USONI KISHA AKAINGIA NAE NDANI KWAKE NA KUMFANYIA UKATILI HUO.
AIDHA
MTOTO AMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUBAINIKA KWAMBA KWELI
AMEINGILIWA KIMWILI, MTOTO YUPO HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, MTUHUMIWA WA UHALIFU HUO AMEKAMATWA, AIDHA
JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, PINDI
UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO
SENGA ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUWA MAKINI
WAKATI WOTE NA WATOTO WADOGO WASIACHWE PEKE YAO ILI KUEPUSHA VITENDO
KAMA HIVI, LAKINI PIA ANAWASIHI WANANCHI KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU
WENYE TABIA KAMA HIZI ILI HATUA STAHIKI ZIWEZE KUCHUKULIWA.
IMETOLEWA NA:
ACP: AUGUSTINO SENGA
KAIMU KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
0 comments:
Post a Comment