Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda jana aliliagiza
jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Gongolamboto, Bakari Shingo baada ya kutuhumiwa kukusanya mapato kwa
kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na Halmashauri
inavyoagiza pamoja na kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu na
kushirikina na wahalifu.
Hatua hiyo ilikuja
baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kukaa muda
mrefu bila kusoma mapato ya mtaa huo pamoja na kughushi stakabadhii za
mapato.
Lawama hizo zilimpelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye alikuwa
kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni kumsweka rumande
Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.
Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif alieleza
kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa
zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia
Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
0 comments:
Post a Comment