Watu
sita wakiwamo mfungwa na wanafunzi wamekufa huku wengine wanane
wakijeruhiwa, baadhi yao vibaya baada ya gari dogo walilokuwa
wakisafiria kuacha njia na kupinduka mara nne katika Kijiji cha Kipande
wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa katika barabara kuu ya Mpanda –
Sumbawanga.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema ajali hiyo ilitokea saa 8.10 jana mchana katika Kijiji cha Kipande.
Aliwataja
waliokufa kuwa ni mfungwa wa Gereza la Kitete lililopo Nkasi, Gaudensi
Nyambo (27), Gasper Malimi (18) na Kenzi Mwambige (18) wote wakiwa
wanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Nkasi na Ofisa
Mipango wa Wilaya ya Nkasi, Godfrey Mwanansao.
Alisema
marehemu wawili hawajatambuliwa huku miili yote ikiwa imehifadhiwa
katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Rukwa ya Mkoa wa Rukwa mjini
Sumbawanga .
“Mfungwa
Nyambo alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Kitete wilayani
Nkasi ambako alikuwa na kesi nyingine mahakamani alikufa wakati
akitibiwa hospitalini hapa,” alieleza Kamanda Kyando.
Alisema
ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Hiace Nissan Vannette lenye namba za
usajili T 966 DHP lililokuwa likiendeshwa na Lusanjo Mwaipopo
aliyekimbia baada ya ajali hiyo.
Alisema
gari hilo lilikuwa likitokea wilayani Nkasi kwenda mjini Sumbawanga
ambapo liliacha njia na kupinduka mara nne kabla halijaanguka ndani ya
gema.
Alisema
chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika huku uchunguzi wa kipolisi
ukiendelea. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dk John Lawi alisema
majeruhi tisa wamepokewa hospitalini hapo ambao mmoja ambaye ni mfungwa
alikufa OPD.
Aliwataja
majeruhi kuwa ni pamoja na askari Magereza wa Gereza la Kitete,
Fortunatus Saanane (44) aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU)
huku hali yake ikiwa tete. Wengine ni askari Magereza, Francis Elay (30)
ambaye alitibiwa na kuruhusiwa.
Kwa
mujibu wa Dk Lawi, majeruhi wengine ni Mbagala Hale, Mamadelwa
Kafadhila, Mathias Mwandaliwa (28) na wengine ambao majina yao
hayakuweza kupatikana mara moja. Alisema hali za majeruhi hao ni mbaya.
0 comments:
Post a Comment