Akizungumza na Mwananchi Digital, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo amesema Kamanda Kakamba amefia hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi Digital iliwasiliana na Kaimu Kamanda Towo kupata uthibitisho wa taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii mapema leo kuwa SACP Kakamba ameaga dunia, baada ya kukosa ushirikiano kutoka kitengo cha mawasiliano cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyokuwa inasambazwa kupitia mtandao wa WhatsApp mapema asubuhi, ilimnukuu Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu akisema: “IGP anasikitika kutangaza kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Peter Kakamba kilichotokea usiku wa saa nne katika Hospitali ya Muhimbili DSM.
Kamanda Kakamba alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa maradhi ya tumbo alikuwa amefanyiwa operesheni hivi karibuni.”
Kwa mujibu wa Towo, mwili wa marehemu Kakamba utawasili Singida kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoani Rukwa kwa ajili ya maziko.
0 comments:
Post a Comment