Mjumbe wa Marekani kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa Samantha Power.
Marekani
imependekeza azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutaka
Sudan Kusini kuwekewa vikwazo vya kununua na kuingiza silaha.
Aidha, azimio
hilo linapendekeza watu binafsi kutoka upande wa serikali inayoongozwa
na rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kuwekewa vikwazo.
Marekani
inasema kwamba kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar, mkuu
wake wa majeshi na waziri wa habari wawekewe vikwazo na Umoja wa Mataifa
kwa kuchochea vita nchini humo.
Kwa
mujibu wa ujumbe uliopatikana na AFP Machar, mkuu wa majeshi ya rais
Salva Kiir, Paul Malong na waziri wake wa habari Michael Makuei wako
kwenye orodha nyeusi ya vikwazo.
Chini ya
hatua iliyopendekezwa, Macha ambaye anapatiwa matibabu nchini Afrika
Kusini na maafisa hao wawili watakabiliwa na vikwazo vya kusafiri na
mali zao kuzuiwa.
Hatua hii
imekuja baada ya watalaam na Umoja wa Mataifa kuonya kuwa huenda
kukatokea kwa mapigano na mauaji ya halaiki nchini humo katika siku
zijazo ikiwa hatua haitachukuliwa.
Azimio
hilo sasa linasubiri kura kutoka kwa wanachama wa Baraza hilo, licha ya
kuwepo kwa wasiwasi huenda Urusi ikatumia kura yake ya Veti na kuzuia
kupitishwa kwa azimio hilo
0 comments:
Post a Comment