Friday, 25 November 2016

Ripoti ya uchunguzi wa mali za BAKWATA yakabidhiwa

...

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber  jana amekabidhiwa ripoti ya awali iliyoandaliwa na tume ambayo ameiunda  kwa ajili ya kufanya uchunguzi  na kuzibainisha  mali zote za  Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Akizungumza wakati wa kumkabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa tume hiyo Sheikh Abubakari Khalid Hajj alisema kuwa  ripoti hiyo imefanyika kwa muda wa miezi mitatu licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa muda.

Aidha aliwambia wanahabari kuwa uchunguzi huo umehusisha ufuatiliaji wa mali za Bakwata katika Mkoa wa Dar es salaam pekee,ikiwemo majengo,viwanja, pamoja na kupitia mikataba mbalimbali ili  kujiridhisha kama imefuata taratibu za kisheria.

Akizungumza mbele ya wanahabari mara baadi ya kupokea ripoti hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber alisema kuwa ataipitia ripoti hiyo  ili kujua yale yaliyobainishwa na tume yake, na kuahidi kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Hata hivyo Mufti huyo ameiongezea muda wa miezi mitatu tume hiyo ambayo ina jumla ya  wajumbe wanane kwa ajili ya kukamilisha kuandaa ripoti ya mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine kwani zoezi hilo litafanyika nchi nzima.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger