Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi wa
reli inayounganisha reli ya kati na kiwanda cha Kiluwa Still Group
cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016 . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZIRI
mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imefanikiwa kuondoa urasimu
katika baadhi ya halmashauri nchini na idara husika katika kutoa hati
miliki kwenye maeneo ya uwekezaji ili kukuza sekta ya uwekezaji.
Aidha
Majaliwa amefarijika kukuta njia ya reli yenye urefu wa km 4.3 kutoka
reli ya kati kuelekea kiwanda cha kutengeneza nondo cha kilua kilichopo
Kibaha Vijijini mkoani Pwani imekamilika kwa asilimia 100.
Sambamba
na hayo amezisihi halmashauri nchini kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji
ili kuongeza ari ya kushawishika kuongeza viwanda.
Majaliwa
aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya kiwanda cha
Kilua cha Mlandizi na kiwanda cha kuunganisha magari na zimamoto cha
Equator suma jkt Ruvu.
Alisema ameridhishwa na hatua zinazoendelea katika kukamilisha ujenzi wa viwanda hivyo.
Majaliwa
alitoa wiki mbili kwa mkandarasi wa umeme katika kiwanda cha kilua
kuhakikisha anakamilisha kufikisha umeme wa uhakika kiwandani humo.
Alieleza
kuwa viwanda hivyo vimefikia kwenye hatua nzuri kwani vimekamilika kwa
asilimia 80 na vyote vinatarajiwa kuanza kazi mapema mwaka 2017.
Hata
hivyo alisema licha ya serikali kuondoa urasimu ulipokuwa ukilalamikiwa
sasa halmashauri ziendelee kutenga maeneo, kupima maeneo ili kufungua
milango ya uwekezaji.
Majaliwa alisema serikali imedhamiria kujenga viwanda na kufufua ambavyo vilikufa .
Aliiupongeza
uongozi wa mkoa wa Pwani kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu
ya tano chini ya rais John Magufuli kujenga viwanda na kuvuta
wawekezaji.
“Kiwanda
hicho ni mradi mkubwa wenye thamani ya zaidi ya bil 200 mara utakapo
kamilika utazalisha tani 2,000 na kuajili ya watu 300-800’
“Awamu
ya kwanza ya kiwanda hiki kimegharimu dola za kimarekani mil. 45 sawa
na sh. bil. 90 za kitanzania, na awamu ya pili kitagharimu zaidi ya dola
milioni 100 sawa na zaidi ya bil 200, mitambo imefungwa na kipo
vizuri,hivyo alimpongeza mwekezaji mzawa Mohammed Kilua”alielezea.
Waziri
mkuu alisema mradi huo utakapoanza kazi utaliingizia mapato taifa kwa
kiasi kikubwa ,kuwezesha ajira kwa wazawa na kuwaingizia kipato
wajasiliamali.
Alisema mkoa wa Pwani unaangaliwa kupeleka viwanda na anashukuru uongozi wa mkoa na kupokea wawekezaji.
Kuhusu kiwanda cha kuunganisha magari na zimamoto Majaliwa alisema ni kiwanda mkombozi nchini.
Majaliwa alisema kwa kuunganisha matrekta na zimamoto kutarahisisha kupata kwa gharama nafuu vyombo hivyo vya moto nchini.
Nae waziri wa uchukuzi, pro. Makame Mbalawa aliomba reli hiyo itumike kwa matumizi lengwa.
Pro.
Mbalawa alielezea viwanda vinavyohitajika njia za reli zinaboreshwa na
kujengwa lakini pia ni jukumu la wawekezaji hao kuzitunza na kuzitumia
vyema.
Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema serikali mkoani
hapo imedhamiria kuongeza wawekezaji na ongezeko la viwanda ili kuongeza
ajira hususan kwa kundi la vijana.
Alisema
wapo baadhi ya wananchi waliotakiwa kupisha reli hiyo ambao wanadai
fidia ya sh. mil 95.726 na halmashauri inadai sh. mil 307.206.
Mhandisi Ndikilo alisema mkoa wanayotaarifa na wanaendelea na mazungumzo ili haki yao walipwe kwa wakati.
Alisema wananafasi kubwa ya kufanikisha nchi kuwa ya viwanda kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanda.
Mhandisi
Ndikilo alisema kuwa kwa sasa mkoa wa Pwani ajenda yake ni kuhakikisha
unakuwa mkoa wa viwanda na hilo linawezekana kwa kuwa na viwanda vingi
vya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa,
alisema waziri mkuu alitoa agizo wakamilishe reli hiyo na sasa
wamemalizia.
Alisema ujenzi huo umetumia sh. Mil 863 kwa kutumia mafundi wa ndani gharama ambayo ni ndogo.
Kadogosa alielezea kwamba wangetumia mafundi wa nje gharama ingekuwa kubwa.
Alisema licha ya kumaliza reli hiyo lakini kiwanda hicho cha kilua kimeomba tena kuongezewa reli nne za ziada.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Mohamed Kilua alisema wanatarajia kujenga kwenye eneo hilo viwanda vingine vinne.
Alitaja viwanda vinavyotarajiwa kujengwa kuwa ni kiwanda cha kutengeneza pikipiki, gemsum, tissues na nguzo za umeme.
Kilua alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kinaliingizia pato taifa bil.25 kwa mwaka na kuzalisha nondo tani 2,000 kwa siku
0 comments:
Post a Comment