1
2
3
4
5
6
7
8
9
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Kocha Mkuu, Zeben Hernandez kulia na Kocha Msaidizi wa Azam FC, Yeray Romero.
............................................................
UONGOZI
wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kwa kushirikiana na
benchi la ufundi la timu hiyo hivi sasa upo kwenye mchakato wa
kukiongezea nguvu kikosi hicho.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa ni nia ya dhati kabisa ya Azam FC kutaka kufanya
vizuri zaidi kwenye mzunguko wa pili wa ligi, Kombe la Shirikisho (Azam
Sports Federation Cup) na michuano ya Kimataifa inayokuja kuanzia mwezi
ujao na mwakani (Kombe la Kagame na lile la Shirikisho Afrika).
Mabingwa
hao wa Ngao ya Jamii mwaka huu, tayari wamemaliza mzunguko wa kwanza wa
ligi wakiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wakijikusanyia jumla ya
pointi 25, wakizidiwa pointi 10 na kinara Simba aliyejizolea 35.
Akizungumza
na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz juzi Kocha Msaidizi wa Azam
FC, Yeray Romero, alisema kuwa kuelekea mzunguko wa pili wa ligi
wanatarajia kuangalia mapungufu ya kikosi hicho kabla ya kuingiza sura
mpya kwenye usajili ya dirisha dogo kwa ajili ya kuinyanyua timu na
kufika kwenye nafasi nzuri zaidi.
“Wakati
wachezaji wapya wanaingia pia tunatarajia kuwaangalia wachezaji ambao
tunadhani kwa sasa kikosini hawawezi kuisaidia timu, ambao ndio
watawapisha wachezaji hao, lengo la yote haya ni kuweza kuipeleka mbele
zaidi timu zaidi ya hapa ilipo,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Romero aliwapongeza wachezaji kwa kazi waliyoweza
kuifanya mpaka sasa huku wao kama benchi la ufundi wakiahidi kufanya
kazi nzuri zaidi kwa asilimia 100 katika kuirekebisha zaidi timu na
kuziba mapungufu yaliyopo.
Matarajio yamefikiwa?
“Kiufupi
matarajio hayakuwepo ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye mzunguko wa
kwanza, hatukuwa tumepanga kufika nafasi hiyo lakini mazingira
tuliyokuwa nayo yametufanya kumaliza hapo, licha ya yote hii ni nafasi
nzuri kwetu na tunachoangalia kwenye raundi ijayo ni kufika nafasi pili
na ya kwanza,” alisema.
Kauli kwa mashabiki Azam FC
Kocha
huyo wa zamani wa timu za CF Reale Juventud Laguna na CD Tenerife zote
za Hispania, aliwashukuru mashabiki wa Azam FC kwa sapoti kubwa
wanayoendelea kutoa kwenye mechi zao licha ya kupitia wakati mgumu
kwenye baadhi ya mechi.
“Kwa
kweli nachukua fursa hii kuwapongeza mashabiki wa Azam FC, kwa yote
yaliyotokea wao wamekuwa pamoja nasi, timu inapofanya vibaya wapo na
inapofanya vizuri wapo na ambacho tunaweza kuwaahidi ni mashabiki wetu
ni kwamba waendelee kuwa na imani na timu yao kwa sababu nafasi
tuliyofikia hivi sasa si mbaya sana, lakini ingawaje si kama ndio
tuliyokuwa tumepanga kufika.
“Hivyo
tunategemea raundi ya pili itakapoanza kwa nguvu ambazo tutaziingiza
kikosini basi wakiwa wanaendelea kutusapoti kama mwanzo naamini ya kuwa
mashabiki watajikuta kwamba hawakukosea kuichagua Azam FC kwa sababu
matokeo yatakuwa ni mazuri kwa timu kuweza kupata ushindi,” alimalizia
mtaalamu huyo.
Azam FC kuendelea kujifua
Wakati
huo huo, mara baada ya kikosi cha Azam FC kurejea jana jioni jijini Dar
es Salaam kikitokea mkoani Shinyanga kilipocheza na Mwadui, taarifa ni
kuwa wachezaji wa timu hiyo wataendelea na mazoezi kama kawaida jioni ya
leo.
Kwa
mujibu wa programu ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Zeben
Hernandez, mara baada ya mazoezi ya leo, kikosi hicho kinatarajia
kucheza mchezo wa kirafiki kesho Jumamosi kabla ya kupumzika Jumapili na
Jumatatu kitacheza mchezo mwingine wa kujipima ubavu.
Tathimini ya mzunguko wa kwanza
Azam FC
inayodhaminiwa na kinywaji safi ya Azam Cola kinachochangamsha mwili na
kuburudisha koo na Benki bora nchini kwa usalama wa fedha zako ya NMB,
imefanikiwa kucheza jumla ya mechi 15 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi
ikifanikiwa kushinda jumla ya mechi saba, sare nne na kupoteza nne ikiwa
imekunja kibindoni pointi 25.
Takwimu
pia zinaonyesha kuwa, Azam FC imeshinda robo tatu ya mechi zake
ilizocheza ugenini, ikiibuka na ushindi mara tano kati ya mechi nane za
ugenini, ikifungwa tatu, kati ya mechi saba ilizokuwa mwenyeji
imefanikiwa kuibuka kidedea mara mbili, sare nne na kuteleza mechi moja.
Hivyo
takwimu hizo zinaeleza kuwa Azam FC imefanikiwa kupata alama 15 kwenye
viwanja vya ugenini kati ya 24 ilizotakiwa kuvuna, ambapo imepoteza
jumla ya pointi tisa ugenini.
Mabingwa
hao wamevuna jumla ya pointi 10 kati ya 21 katika uwanja wa nyumbani,
ikiwa imeacha uwanjani jumla ya pointi 11, nane katika uwanja wake wa
Azam Complex kutokana na sare nne ilizotoa ndani ya dimba hilo na tatu
ikiziacha ndani ya Uwanja wa Uhuru kufuatia kupoteza bao 1-0 dhidi ya
Simba ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 35 pungufu ya pointi 10 na
mabingwa hao.
Rekodi ya
ufungaji wa mabao zinaonyesha kuwa mpaka sasa kikosi hicho kimefunga
21, ukiwa ni wastani wa bao 1.4 kwenye kila mchezo katika mechi 15
ilizocheza huku pia ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 14 (yaani
wastani wa kufungwa bao 1.0 kwenye kila mchezo iliocheza).
Nahodha
John Bocco ‘Adebayor’, ndiye ameonekana kinara wa kutupia mabao msimu
huu ndani ya Azam FC mpaka sasa akitupia sita akizidiwa mabao matatu na
Shiza Kichuya wa Simba aliyekuwa kileleni kwa mabao tisa, wengine
wanaomzidi ni Rashid Mandawa (Mtibwa Sugar), Simon Msuva, Amissi Tambwe
(Yanga), ambao wote wamefunga saba kila mmoja.
Bocco pia
yupo kileleni kwenye utengenezaji wa mabao akiwa ametoa pasi za mwisho
nne, akifuatiwa kwa ukaribu na Khamis Mcha aliyechangia matatu ambaye
pia ametupia wavuni matatu, huku Shaaban Idd aliyeweka kambani matatu
naye akipika mawili.
Mpaka
raundi ya kwanza inamalizika mchezaji wa Azam FC aliyecheza mechi nyingi
kuliko mwingine yoyote ni kipa namba moja, aliyecheza 14 sawa na dakika
1,260 kati ya 1,350, alizotakiwa kucheza hadi ligi inafikia katikati na
hii ni baada ya kupumzishwa mechi moja wakati kikosi hicho
kikikabiliana Mbao, mchezo ulioisha kwa Azam FC kuteleza kwa kufungwa
mabao 2-1. (P.T)
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambae pia ni katibu wa kamati ya
usalama barabarani mkoani Pwani,Abdi Issango,(aliyeshikiwa
mic)akionekana anazungumza jambo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WATUNGA
sera kupitia serikalini wameombwa kuangalia uwezekano wa kuzifanyia
marekebisho baadhi ya sheria za usalama barabarani ikiwemo adhabu za
faini zinazotolewa ziweze kuwa na maumivu kwa wakiukwaji.
Watunga
sera hao wanatakiwa kuzipitia upya sheria hizo (The road traffic act cap
168) ya mwaka 1973 kwani kifungu cha 50 kulipita gari vibaya adhabu
yake ni sh 1,000 na isizidi 2,000 na kifungu cha 45 dereva aliyekutwa
amelewa ni sh.10,000 hadi 20,000.
Kamanda
wa usalama barabarani mkoani Pwani, Abdi Issango ,aliyasema hayo wakati
akizungumza na wadau wa usalama barabarani na waandishi wa habari.
Alisema
baadhi ya sheria ni za zamani hivyo zinapaswa kwenda na wakati na haina
budi ziangaliwe upya kwa kubadilishwa ili kwenda na hali ilivyo sasa.
Kamanda
Issango alieleza kwamba sheria hizo husababisha baadhi ya watumiaji
barabara hususan madereva kutokuwa na hofu ya kukiuka sheria kutokana na
faini kuwa ndogo.
“Mfano wa
sheria ya usalama barabarani (The Road Traffic Act Cap 168) ya mwaka
1973 adhabu nyingi ni ndogo na hazileti majuto wala hofu kwa mkosaji ,
ni kinyume na malengo ya adhabu ya kumpa maumivu mhusika”
“Kifungu
cha 50 cha kulipita gari jingine vibaya adhabu yake ni sh. 1,000 na
isizidi sh.2,000 na kifungu cha 45 dereva akitiwa hatiani kwa kosa la
ulevi adhabu yake ni sh.10,000 na isizidi 20,000,” alisema Issango.
Alifafanua
adhabu inatakiwa mkosaji apate majuto,hofu na maumivu ili ajutie kosa
na kuogopa kosa alilotenda, hivyo kutokana na adhabu hizo kuna haja ya
kuzipitia upya sheria hizo ili zitoe adhabu kali.
Issango
ambae pia ni katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoani hapo alitoa
rai kwa jamii na wadau mbalimbali kuipigia kelele serikali ili iweze
kubadilisha baadhi ya vifungu vinavyotoa adhabu ndogo kwa wakosaji .
Alieleza
endapo adhabu zitakuwa kubwa itasababisha kuogopa ama kusita kurudia
makosa kwa makusudi kwani wengine wanarudia kwa kujua adhabu siyo kali.
Issango
alisema katika kukabiliana na ajali mahakama zinapaswa kutenda haki na
kumaliza kwa wakati kesi zinazotokana na usalama barabarani .
Alisema pia wadau wote wanapaswa kushirikiana ili kupunguza ajali ambazo nyingine zimekuwa zikisababishwa kutokana na uzembe.
“Nawasihi
madereva wa vyombo vyote vya moto kuacha kufanya mbwembwe wakiwa
barabarani ,kutotumia vilevi wakati wakiendesha ,kuacha kupita magari
mengine(overtake)ovyo na mwendo kasi ili kuepukana na ajali”anasisitiza . (P.T)
.Mwalimu
wa Ufundi Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na
waandishi wa habari juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo
ya ufundi Stadi.
Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiwa katika mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi
Mwalimu wa uChuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunnzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari.
Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha watanzania tamaduni ,mila na desturi ili kuulinda utamaduni wetu , ambao unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku.
Akizungumza
na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu
wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania .
Amesema
utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya
utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi
duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
Amesema chuo chake kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Communinity College cha nchini Canada kinaanda kozi hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali.
Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza kutolewa.
Aidha
mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo
wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia
technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala.
Ayo
amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka
katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa
na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
Ametoa
rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro
kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa
sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na
serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka
msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda. (P.T)
ALIYEKUWA
MKUU WA MAJESHI JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA AKIZUNGUMZA NA
WAANDISHI WA HABARI (Hawapo Pichani ) KATIKA KLABU YA GOLF YA JESHI LA
ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM KUHUSU
MAANDALIZI YA KOMBE LA WAITARA LINALOTARAJIWA KUGOMBANIWA JUMAMOSI
NOMVEMBA 19 (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
BAADHI YA
WANAFUNZI WALIOJITOKEZA KUPATA MAFUNZO YA MCHEZO WA GOLF KATIKA KLABU
YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR ES
SALAAM WA KWANZA ALIYEPIGA MPIRA NI LUTENI FADHILA NAYOPA (Picha na
Luteni Selemani Semunyu)
ALIYEKUWA
MKUU WA MAJESHI JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA AKIZUNGUMZA NA BAADHI
YA WANAFUNZI WALIOJITOKEZA KUPATA MAFUNZO YA MCHEZO WA GOLF KATIKA KLABU
YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR ES
SALAAM.(Picha na Luteni Selemani Semunyu)
MCHEZA
GOLF NICHOLOUS CHINDA AKIMFUNDISHA NAMNA YA UKAAJI MMOJA WA WANAJESHI
WALIOJITOKEZA KUJIFUNZA MCHEZO HUO KATIKA KLABU YA GOLF YA LUGALO
JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
BAADHI YA
WANAFUNZI WALIOJITOKEZA KUPATA MAFUNZO YA MCHEZO WA GOLF KATIKA KLABU
YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA YA LUGALO JIJINI DAR ES
SALAAM WAKIANGALIA NAMNA YA UPIGAJI MPIRA (PICHA NA LUTENI SELEMANI
SEMUNYU).
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mstaafu George Waitara amesema wakati umefika sasa kwa Michezo ya Majeshi
kwa nchi za Afrika Mashariki kujumuisha mchezo wa Golf kutokana na
idadi kubwa ya maofisa na Askari wanaojitokeza kucheza mchezo huo katika
Nchi hizo.
Aliyasema hayo Leo Jijini
Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kufuatia kuanza
kwa Maandalizi ya Kombe la Waitara linalotarajiwa kufanyika Novemba 19
Mwaka huu katika Viwanja vya Jeshi vya Lugalo.
“Ukiangalia Uongozi mpya na mkakati iliofanya na idadi kubwa ya Maofisa na Askari walioanza kujitokeza kujifunza mchezo huo ni
ishara tosha kuwa wakati umefika kwa mchezo huo kuingizwa katika
michezo itakayoshindaniwa katika Michezo ya majeshi kwa kuwa na nchi
nyingine pia wapo,Alisema Jenerali Waitara.
Aliongeza kuwa ni
furaha yake ikiwa ni miaka kumi tangu kuanzishwa na mwitikio kuwa
mkubwa hivyo anaimani miaka ijayo kutakuwa na idadi kubwa zaidi na hivyo
kuomba waaandishi wa habari kuendelea kuutangaza mchezo huo.
Akizungumzia
Maandalizi ya Mashindano ya Kombe lake aliahidi kikundi chake
kinachocheza ndani ya Klabu ya Lugalo na “Generals Four Balls” kitafanya
vizuri katika mashindano hayo licha ya umri mkubwa walionao.
Aliwataja washiriki wa Kikundi hicho kuwa ni Yeye Binafsi Jenerali Mstaafu Waitara,
Balozi Charles Sanga , Dk Edmund Mndolwa na Katibu Mkuu wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima na kuwataka wengine pia
kuanzisha vikundi vya Ushindani ndani ya Klabu ili kuongeza hamasa.
Jenerali Waitara aliwataka wachezaji wengi kujitokeza kushiriki katika mashindano
hayo kutokana na historia yake lakini kupunguza gharama kwa wachezaji
kwa kuwa uwanja pekee wa kizalendo nchini huku gharama zikiwa chini ukilinganisha na viwanja vingine.
Kwa Upande Wake Balozi Charles Sanga alishukuru JWTZ kwa kuamua kuanzisha uwanja lakini pia kwa mwanzilishi wa Uwanja kutokana na Ukweli kuwa Uwanja Wa Golf wa Lugalo umekuwa kimbilio kwa Watu wote kutokana na uzuri wake na gharama kuwa za chini. (P.T)
Hivi
ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General
Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la
Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.
Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari
Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa
ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka
moto utakapozimwa kabisa
Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika
Mmoja wa
waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani
akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa. (P.T)
UK Tanzania Diaspora summit UK 2016
TANGAZO LA MDAHALO KUHUSU ARDHI TANZANIA
Wana
Diaspora wa UK manalikwa kuhudhuaria kongamano litakalojadili
mstakabali mzima wa haki ya Mwana Diaspora kikatiba ikiwemo haki ya
kumiliki ardhi Tanzania iwapo wewe ni mzawa.
Mdahalo unatarajia kutoa elimu na mapendekezo juu ya swala hili. Patakuwepo na wataalam mbalimbali wa maswala haya.Karibu University of Coventry, School of Engineering
TAREH 3 December 2016
Saa 4 asubuhi
Uwepo wenu ni mhimu. Umoja ni nguvu
Kwa tarifa zaidi walisiliana na simu +44 7960811614
Ahsanteni
WOTE MNAKARIBISHWA (P.T)
Na Daudi Manongi, MAELEZO
Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL) imekusanya shilingi bilioni 8.1 katika robo ya
kwanza ya mwaka 2016 ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 1.6 ya robo ya
kwanza ya mwaka 2015 ambapo ilipata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni
6.5.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw.Masanja Kungu Kadogosa wakati
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Bwana
Masanja anasema kuwa huduma ya usafirishaji abiria imezalisha mapato ya
wastani wa shilingi bilioni 1.1 katika kipindi cha mwaka 2016 na Wastani
wa shehena kwa robo mwaka imeongezeka na kufikia tani 63,251
ukilinganishwa na tani 48,681 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho
mwaka jana.
Aidha
kati ya mwezi Juni hadi Octoba mwaka 2016 kampuni imetekeleza miradi
midogo kadhaa ya kujenga michepuo ya reli kwenda kwenye viwanda vya
wateja wa TRL wenye kuzalisha shehena,ambapo Baadhi ya miradi ya reli za
michepuo zilizojengwa ni kwenda kiwanda cha mbolea cha Yara kilichopo
Kurasini na kiluwa Group ya Mlandizi huku michepuo mingine inatarajiwa
kujengwa kuelekea viwanda vya Saruji vya Rhino na Sungura vilivyopo
mkoani Tanga.
Aidha
Bw.Kadogosa amesema kuwa wamefanikiwa kufanya ukarabati wa mabehewa ya
mizigo 120 yaliyogharimu shilingi milioni 700 na kusema kama
yangefanyiwa ukarabati nje ya nchi yangegharimu shilingi bilioni 26.
Mbali na
hayo menejimenti ya TRL inaendelea kutoa kipaumbele katika kutatua madai
ya wafanyakazi wake ikiwemo kuwasilisha Michango katika mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya(NHIF),WADU na Saccos NMB ambapo baada ya kuwasilisha
makato wafanyakazi wameanza kupata huduma stahiki.
Aidha
malimbikizo ya nyongeza ya mshahara yameshatengewa shilingi milioni 600
ambazo zimelipwa ikiwa ni awamu ya tatu na menejimenti inajipanga
kumaliza awamu nyingine zilizosalia.
Mkurugenzi
huyo ametoa wito kwa wadau na wananchi kuhakikisha wanalinda
miundombinu ya reli na kuripoti mara moja kwenye vyombo vya dola wale
wote wanaohujumu miundombinu kwa manufaa binafsi.(P.T)
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu hoja
mbalimbali za wabunge katika mkutano wa tano wa Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.
Benki Kuu
ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali
za kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la
dunia na kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya
rasilimali ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe.
Dalaly Kafumu aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza
dhahabu safi katika Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo
inayozalisha dhahabu safi.
Mhe.
Kijaji amesema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na
kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya
ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki
Kuu inadhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali
zikiwemo za kuuza dhamana na hati fungani za Serikali pamoja na
kushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni kati ya mabenki.
“Katika
kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali
za kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua
miezi minne lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki
dhahabu kama sehemu ya rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya
dhahabu katika soko la dunia”, alisema Mhe. Kijaji.
Naibu
Waziri huyo ametoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la
Dunia ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika
mwezi Septemba 2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba
2015.
Mhe.
Kijaji amefafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa
dhahabu – fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu
hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya
kudumisha thamani, wepesi wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana
kwa kuwekeza hazina hiyo.
Aidha,
Mhe. Kijazi amesema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu
unahitaji ujuzi maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki
Kuu inaonyesha dhahiri kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo
la biashara ya madini hayo. (P.T)
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza
waombolezaji katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani
na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Mze Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais
Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick
Sumaye Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Mama Salma Kikwete
jana Novemba 10, 2016 PICHA NA IKULU
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Kaka
wa marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji
mjane wa marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji
mtoto wa marehemu, Jimmy Mungai, baada ya kutoa heshima zake za mwisho
kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji
mtoto wa marehemu William Mungai marehemu baada ya kutoa heshima zake za
mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph
Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10,
2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wanafamilia
baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa
Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es salaam jana Novemba 10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wanafamilia
baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa
Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es salaam jana Novemba 10, 2016
Sehemu ya
familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai
katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es salaam jana Novemba 10, 2016 (P.T)
More...
Tafuta Habari
Nafasi za Kazi & Masomo
Prev
Next
Video Gallery
Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.
Maoni ya Wanakijiji
-
PINDA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA
06.11Napenda namna ya Pinda, kwamba ulipewa nafasi ya kutenda kipindi chako kimeisha kaa zako pembeni ... -
Tafadhali Uninukuu....
04.11Majid, ningefurahi kama ungetuonyesha japo nyumba 2 au tatu za wanakijiji cha Mputa ambako wanafunzi ... -
Mwaka Mmoja Wa Magufuli Na Kama Urais Ungekuwa Wa Mwaka Mmoja
01.11Upo sahihi kaka Maggid -
TUPSE: WAAJIRI NCHINI WANATAKIWA KULIPA MAPUNJO YA MISHAHARA KWA WAFANAYAKAZI
29.10Tatizo la TUPSE chama hiki kimekaa kiutapeli ndo maana walinzi wengi hawapendi kujiunga mimi nilikua ... -
Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli ya Kitalii katika Kijiji cha Matemwe Zanzibar Inayojengwa na Pennyroyal
25.10Hello there Can I have some contact for pennyroyal company, i am interest to propose them some ...
0 comments:
Post a Comment