Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhamishia Bodi ya Pamba katika
Mkoa wa Mwanza kabla ya Novemba 10 mwaka huu ili kuhakikisha wakulima wa
pamba waliopo katika mkoa huo wanapata huduma zilizo bora kwa ukaribu
na haraka.
Hayo
yamesemwa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.
William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto
Biteko lililohoji juu ya hatua ya Serikali kwa wakulima walioathirika
na pembejeo zilizotolewa ambazo hazikuwa na ubora pamoja na kuhamishia
Bodi ya Pamba katika mkoa huo.
”ili
kuwafikia kirahisi wakulima wa pamba waliopo mkoani Mwanza, Wizara
imeamua kuhamishia Bodi hiyo katika mkoa huo na kwa taarifa zilizopo
Bodi hiyo inatakiwa kuhama haraka iwezekanavyo kabla ya Novemba 10 mwaka
huu”, alisema Mhe.Ole Nasha.
Kwa
upande wa matatizo ya pembejeo, Mhe. Ole Nasha alisema kuwa Serikali
tayari ina taarifa kuhusu tatizo lililowapata wakulima wa pamba katika
maeneo mbalimbali kwa kusambaziwa viuatilifu pamoja na mbegu ambazo
hazikuwa na ubora unaotakiwa hivyo kuathiri wakulima nchini.
“Serikali
iliiagiza Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) kufanya
uchunguzi wa malalamiko ya wakulima ambao ulibaini kuwa viuatilifu hivyo
vilikuwa na utendaji hafifu hivyo Serikali itaanza kuzalisha mbegu bora
za pamba za UK08 ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena”, alisema Mhe. Ole Nasha.
Naibu
Waziri huyo amefafanua kuwa kufuatia changamoto hizo za uotaji wa
mbegu, Serikali iliamua kufanya majaribio ya utoaji wa mbegu ambazo
zilikuwa zikisambazwa hapo awali bila kujua ufanisi katika uotaji wake.
Alithibitisha
kuwa, matokeo ya jaribio hilo yamewezesha kutoa maelekezo kuhusu aina
za mbegu za pamba zenye sifa za msingi ambazo zitasambazwa kwa wakulima
katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017.
0 comments:
Post a Comment