Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni ametangaza vita dhidi ya majambazi na watu wanaojihusha na mauaji.
Alisema Serikali imelazimika kutangaza vita hivyo baada ya kutokea matukio 41 yaliyohusisha mauaji ya kinyama tangu Januari hadi mwezi uliopita.
“Serikali
ipo kazini, sasa inatangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na
ujambazi, watakaobainika hakika wataangamizwa hatuwezi kukubali watu
wazidi kupoteza maisha pasipo na sababu za msingi,” alisema Masauni.
Waziri
huyo alitembelea Msikiti wa Rahman Mtaa wa Utemini Kata ya Mkolani
wilayani Nyamagana, Mwanza na kusema matukio hayo yanapaswa kutokomezwa
na kukemewa kwa nguvu zote.
“Mauaji hayo yalikuwa ya kutisha hivyo ilikuwa ni lazima watuhumiwa wakamatwe, hata hao waliokimbia wanapaswa kutiwa mbaroni,” alisema.
Pia, alionya tabia ya baadhi ya polisi kujihusha na vitendo vya uhalifu na kupoteza imani na uaminifu kwa wananchi.
Aliwataka polisi wanaofanya vitendo hivyo kuacha na badala yake wapambane na wahalifu.
Masauni
alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa utulivu,
hivyo haitakubali watu wachache kuvuruga amani iliyopo
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema vyombo vya usalama vipo imara
kwani baadhi ya wahalifu wameuawa na wengine kukamatwa na wanaendelea
kuhojiwa.
Mjumbe
wa baraza la masheikh Wilaya ya Nyamagana, Saidi Darwesh alisema tukio
la mauaji ya msikitini limesababisha hofu kwa waumini, hususan kipindi
hiki cha mfungo wa Ramadhani kwani wengine hawaendi msikitini kuswali.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Utemini, Jukael Kiula alisema wakazi wa Kata ya
Mkolani wamejitolea kujenga kituo cha polisi katika mtaa huo ili
kudhibiti uhalifu unaotokea mara kwa mara.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili
kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed
Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani
humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini
huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili
kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
(kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na
waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na
majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mzee
wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati
(kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi
ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni
rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika
mauaji hayo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akimpa pole askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na
majambazi wakati wa mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika
mapango ya utemini, jijini Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati
ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi ya Mabatini, jijini humo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment