Akizungumzia tuhuma hizo za wizi, Detail
alisema Drake alimuibia mdundo huo mwaka 2014 walipokuwa na makubaliano
ya kufanya kazi pamoja lakini yakavunjika na kuanzia hapo amekuwa
akimtaka rapa huyo asiutumie mdundo huo lakini yeye amekaidi.
“Nimemfikisha mahakamani Drake maana
amekaidi makubaliano yetu baada ya kushindwa kufanya kazi pamoja.
Kiukweli hakuwa mstaarabu na hili litakuwa fundisho kwa rapa wengine
wenye tabia kama yake ambao wanafikiri mkono wa sheria hauwezi kuwagusa
kwa vile tu wana majina makubwa,” alisema Detail.
Hata hivyo, Drake na Detail waliwahi
kuwa na ugomvi mkubwa mwaka 2014 baada ya kushindwa kufanya kazi pamoja
na kupigana huku chanzo haswa cha ugonvi wao kikiwa hakijawekwa wazi.
0 comments:
Post a Comment