Wabunge
wanatarajiwa kukatwa asilimia 30 ya kiinua mgongo chao ambacho kimeelezwa kuwa
ni Sh200 milioni. Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye Kamati ya Bajeti
iliyopitia muswada huo, zimeeleza kuwa asilimia hiyo inatokana na marekebisho yaliyofanywa na
kupitishwa na wabunge wenyewe kwenye Sheria ya Mapato ya 2010. “Marekebisho ya
asilimia 30 yalifanyika 2010 lakini huu muswada wa sasa unafuta msamaha hivyo,
wabunge watakatwa kodi ya asilimia hiyo ambayo ni sawa na Sh60 milioni kila
mmoja,” kimeeleza chanzo chetu. Alipoulizwa kuhusu makato hayo Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema
anayeweza kuzungumzia mambo ya Kamati ya Bajeti ni mwenyekiti wa kamati
hiyo, Hawa Ghasia. Hata hivyo, Ghasia alipoombwa kutoa ufafanuzi huo, ameeleza
kuwa kamati yake bado inaendelea na kazi
0 comments:
Post a Comment