Stori:
MKALI katika gemu la
Muziki wa Hip Hop, Bongo, John Saimoni ‘Joh Makini’ amefunguka kuwa
serikali inatakiwa kuhakikisha inaweka mkazo katika sheria yake
inayowataka watu wasifanye uhalifu wa aina yoyote mtandaoni hasa wale
wanaotumia elimu yao ya masuala ya mtandao kuwanyanyasa wengine kwa
‘kuhaki’ akaunti zao za mitandao ya kijamii kisha kuzitumia wanavyotaka
wao.
Akichonga na gazeti hili Joh alisema
amekumbana na kisanga cha kuchukuliwa akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii
wa Instagram hivi karibuni jambo lililompa usumbufu wa kuhakikisha
anairudisha tena akaunti hiyo mikononi mwake ambayo kwake ni ofisi kwa
sababu ni sehemu anayokutana na mashabiki wake kwa urahisi.
“Serikali inatakiwa kuliangalia suala
hili kwa mkazo zaidi kwa sababu bado uhalifu wa mitandao unasumbua watu
wengi na unasababisha mpaka wengine wanapoteza pesa bila sababu yoyote.
Hivi karibuni nilichukuliwa akaunti yangu na imenilazimu kupambana
kuirudisha kiasi kwamba nimebadilisha mpaka jina,” alisema. John Makini.
0 comments:
Post a Comment