Wabunge
wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo wametumia mtindo mpya kueleza hisia
zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wamejifunika
midomo kwa karatasi.
Hii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Mbunge
wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo
huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.
0 comments:
Post a Comment