Usiku wa June 19 kuamkia 20 ilikuwa ni
siku ambayo mashabiki wa soka la bongo, wanasubiri kwa hamu kuangalia ya
kwanza ya hatua ya nane bora kati ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Stade de I’Unite Maghrebine wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 19000.
Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Yanga wa Kundi A lenye timu za TP Mazembe ya Kongo, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, katika mchezo huo Yanga wamekubali kufungwa jumla ya goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Yacine Sahli dakika ya 20 ya mchezo ila Yanga walipata pigo baada ya Mwinyi Haji kuoneshwa kadi nyekundu kwa kucheza faulo.
Kwa matokeo hayo Yanga ambayo inasubiri kucheza mchezo wake wa pili wa Kundi A dhidi ya TP Mazembe June 28 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na TP Mazembe wenye point tatu na magoli matatu, wakifuatiwa na MO Bejaia wenye point tatu wametofautiana magoli ya kushinda na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment