Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa angebaki ndani ya chama hicho
wangekuwa na mzigo mkubwa wa kuwaaminisha watu kuwa CCM si mafisadi. Akizungumza
katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma hivi karibuni Nnauye
amesema: “Yeye alikuwa alama ya ufisadi alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu
walikuwa wanahusisha ufisadi na umaskini, walichoka na walikuwa radhi kuchagua
hata jiwe lakini si CCM.” “CCM ilifika pabaya, kelele zilizidi kwani tuhuma
dhidi yake (Lowassa) zilikuwa zikikipaka matope chama. Wananchi walikuwa
wameichoka Serikali yao kutokana na kuingia mikataba mibovu, rushwa, ufisadi na
watu walikuwa wanafanya vitendo vya aibu na kujificha ndani ya chama.
0 comments:
Post a Comment