TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya
Serikali (TSN).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.
Kabla
ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti
ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
21 Juni, 2016
0 comments:
Post a Comment