Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amewataka watumishi wa Taasisi hiyo kuendelea kuwa wabunifu na wachapa kazi zaidi katika utoaji wa huduma kwa wananchi hususan waombaji kazi ambao wamekuwa wakikutana nao katika uendeshaji wa mchakato wa Ajira.
Amesema hayo leo wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wote wa Taasisi hiyo ikiwa ni utekelezaji ratiba yake katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu, ambapo siku ya tarehe 21 Juni, 2016 ofisi hiyo iliitenga kama siku maalum ya kukutana na wananchi kwa ajili ya kupokea hoja na maswali mbalimbali na kuyapatia ufumbuzi.
''Pamoja na yote tuliyozungumza lakini ningefurahi zaidi endapo kila
mmoja wetu anapokuja kazini kila siku anafanya kazi kwa ubunifu na
kujituma akitambua huduma tunayotoa inagusa maisha ya watu na pia
inahitaji mtu mwenye maadili, anayejali muda, mbunifu na mchapakazi ili
kuweza kuleta tija kwa Taasisi na wale tunaowadumia'' alisema Daudi.
Aidha, aliwapongeza watumishi hao kwa kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hali iliyopelekea Sekretarieti ya Ajira kushika nafasi ya kwanza katika uzingatiaji wa maadili, kati ya Taasisi za Umma ishirini (20) zilizokaguliwa na Idara ya Ukuzaji wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
''Ni jukumu letu kama taasisi kutathimini ushindi huu na kuufanya kama chachu ya kuendelea kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika kutekeleza majukumu yetu ili tuweze kuongoza tena mwakani'' alisisitiza Daudi.
Katibu huyo alihitimisha kikao hicho kwa kuishukuru Menejimenti na Watumishi wote kwa ushirikiano, kwa hoja na michango waliyotoa, akiamini yale yote waliojadiliana yanalenga kuboresha utendaji kazi wa mtu mmoja mmoja na Taasisi kwa ujumla ili kuweza kuisaidia Serikali kutimiza malengo iliyojiwekea.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

source: ajira.go.tz
0 comments:
Post a Comment