Wakazi wa
Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga wanatarajia kupata umeme kutoka mgodi wa
Buzwagi. Hayo yalisemwa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya
ya Kahama, Sule Kabati amesema hayo alipokuwa akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya
hiyo, Vita Kawawa aliyetembelea mradi wa mtambo wa kuunganisha umeme kutoka
katika mgodi huo. Meneja huyo alisema kuunganishwa na kuwashwa kwa mtambo huo
kutamaliza tatizo la kukatika umeme uliokuwa ukiukabili mji huo na vitongoji
vyake. “Pia, mtambo huu utaongeza uwezo wa Tanesco wa kuhudumia wateja wengi
zaidi kulinganisha na awali,” amesema Kabati. Umeme huo unatarajiwa kuwashwa
Juni 24, mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment