STORI: BONIPHACE NGUMIJE
DIVA anayefanya poa kwa sasa
kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Vannesa Mdee ‘V-Money’ hivi
karibuni anategemewa kusikika kwenye kolabo mpya aliyopiga na wasanii
kutoka Kenya wanaounda Kundi la Sauti Sol.
V-Money aliiambia safu hii kuwa, kolabo
hiyo ambayo bado hajawa tayari kuvujisha jina lake ni ya pili kwake
kufanya na wasanii wa nje kwa siku za hivi karibuni baada ya ile
aliyofanya na 2Face Idebia kutoka Nigeria ambayo pia bado haijaachiwa
rasmi.
“Nimefanya kolabo hivi mbili siku za
karibuni na wasanii wa nje, nategemea zitaniongezea ujazo kwenye ‘fun
base’ yangu kwa sababu wasanii ambao nimefanya nao kazi, wote wanafanya
vizuri Afrika, pia wana mashabiki wengi,” alisema V- Money.
0 comments:
Post a Comment