WAZIRI
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
ametangaza kiama kwa watendaji wote wa Bodi ya Mikopo waliofanya
ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu
wasiohusika.
Joyce ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa bodi ya mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum katika hoja 17 ni
hoja moja imepata majibu na kuzaliwa dosari zingine ambazo ni kutokuwa
na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watu ambao wanarejesha mikopo.
Amesema
kuwa kutokana na matatizo ya bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha
wanachukua hatua kwa watendaji wote waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha
vyombo vya dola.
Joyce
amesema kuwa katika dosari nyingine wanafunzi zaidi ya 2,000 wamepewa
mikopo katika vyuo viwili lakini wanafunzi hao hawapo katika vyuo
vilivyotajwa.
Amesema
kuwa kuna wanafunzi wanalipwa sehemu mbili ya mikopo ya bodi kwa
Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati
mikopo kabisa na ni watoto wa masikini.
Aidha
amesema bodi hiyo inatakiwa kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua
ambazo wamezichukua kwa baadhi ya watendaji ambao wamefuja fedha za
walipa kodi.
Joyce
amesema kuwa matatizo mengine ni Baraza la Usajili wa vyuo vya Elimu
na ufundi (NACTE) kufanya kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo
ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.
Amesema yote wanaangalia kwa kupitia sheria na kuona jinsi ya kuboresha utendaji kazi kwa NACTE
0 comments:
Post a Comment