Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Kanda ya Pwani kimesema kinatafakari hatua gani ya kuchukua
baada ya Rais John Magufuli kutaka siasa za nguvu zifanywe wakati wa
Uchaguzi Mkuu ujao, kauli inayotafsiriwa kuwa ni kupiga marufuku
shughuli za kisiasa.
Rais alitoa kauli hiyo mapema wiki iliyopita
wakati akipokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) na kuisisitizia juzi wakati wa hafla ya kuzindua mpango
wa polisi wa kuboresha huduma za usalama wa jamii.
Akizungumza jana
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, katibu wa Chadema wa kanda hiyo, Casmir
Mabina alisema wamefikia azimio la kupinga unyanyasaji na ukandamizaji
kwa vyama vya siasa unaofanywa na Serikali ya Dk Magufuli.
Mabina
alisema Rais Magufuli anavunja Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya
mwaka 1992 ambayo inaviruhusu vyama vya siasa kuendesha shughuli
mbalimbali za kisiasa.
Alisema vyama haviwezi kukaa kimya mpaka mwaka
2020 wakati kazi yao ni kukutana na wananchi.
“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe ... afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina.
“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe ... afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina.
Mabina aliongeza kuwa Jeshi la Polisi liache kutumiwa
na Serikali kufinyanga sheria za nchi na kukandamiza upinzani kwa
kutumia vibaya Sheria ya Jeshi la Polisi, kifungu cha 43 (3) kwa
kusingizia habari za ‘kiintelijensia’ na ‘hali ya uvunjifu wa amani’.
Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Dar es Salaam Kuu, Mwita Waitara
alilalamikia kitendo cha mameya wa Dar es Salaam kunyimwa vibali vya
kwenda nje ya nchi kutafuta fedha ili kusaidia maendeleo ya halmashauri
zao.
Alisema fedha za safari hizo zinatolewa na washirika wa maendeleo,
lakini Serikali imekuwa ikizuia safari hizo kwa kisingizio cha kubana
matumizi.
Alisema safari nyingine za nje ni muhimu kwa sababu
zinawawezesha mameya kukutana na wadau wa maendeleo ili kupata misaada.
“Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alikuwa na safari ya kwenda Afrika
Kusini kukutana na mameya wengine duniani, lakini alizuiliwa kwa
maelekezo.
"Hatuwezi kuendelea kama tutashindwa kukaa na wenzetu ili
kujifunza mambo ya maendeleo,” alisema.
Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM.
Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM.
Alisema yeye pia alizuiliwa kwenda Marekani akiwa mjumbe wa Kamati ya
Bunge ya Huduma za Jamii.
Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa.
Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa.
Dk
Mahanga alimtaka Rais akumbuke ahadi mbili alizozitoa wakati wa kampeni
na wakati anaapishwa, ambazo ni kuilinda Katiba na kuwaletea wananchi
maendeleo.
“Kinachowaogopesha CCM ni upinzani kupata kura zaidi ya
milioni sita wakati wa uchaguzi. Wanajua kwamba wanaweza kuchukua nchi,
ndiyo maana wameanza kudhibiti vyama vya siasa ili visiwe na nguvu,”
alisema Dk Makongoro ambaye aliwahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu
ya Nne.
0 comments:
Post a Comment