TAREHE
20/06/2016 MAJIRA YA SAA 07:30HRS KATIKA MSITU WA BUHINDI ULIOPO KIJIJI
CHA MAJENGO KATA YA IRENZA TARAFA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA
MWANZA, MARIAM MATHIAS MIAKA [35] MKAZI WA KIJIJI CHA NYANGALAMILA
ALIKUTWA AKIWA AMEKUFA KIFO CHA MASHAKA KATIKA MSITU TAJWA HAPO JUU HUKU
UCHUNGUZI WA AWALI UKIONYESHA MWILI WAKE UKIWA NA MIKWARUZO KWENYE BEGA
LA KULIA PAMOJA NA SHINGO.AIDHA
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE SIKU YA IJUMAA YA
TAREHE 17.06.2016 MAJIRA YA ASUBUHI NA KWENDA KATIKA MSITU TAJWA HAPO
JUU KUTAFUTA KUNI NA NDIPO MAUTI YALIPO MKUTA HUKO, HADI TAREHE
20.06.2016 MAJIRA YA SAA 07:30HRS AMBAPO MWILI WAKE ULIWEZA KUOKOTWA
KATIKA MSITU HUO.
JESHI
LA POLISI LINAMSHIKILIA MUME WA MAREHEMU AITWAYE PONYIWA JEREMIA MIAKA
[37], MKAZI WA NYANGALAMILA KWA MAHOJIANO ZAIDI DHIDI YA TUKIO HILO
KWANI ALISHINDWA KUTOA TAARIFA POLISI NA KWA MAJIRANI ANAOISHI NAO KWA
KIPINDI CHOTE AMBACHO MKEWE HAKUONEKANA NYUMBANI KWAKE HIVYO KUPELEKEA
KUTILIWA SHAKA KATIKA TUKIO HILO.
CHANZO
CHA KIFO HICHO BADO HAKIJAJULIKANA, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA
UCHUNGUZI PAMOJA NA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA
MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU
WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA WAONGEZE USHIRIKIANO KWA JESHI
LA POLISI WAKATI WOTE PANAPOTOKEA JAMBO AU TATIZO WASISITE KUTAARIFU
ILI KUWAZA KUZUI VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA
TAREHE 20.06.2016 MAJIRA YA SAA 13:20HRS NA KUENDELEA KATIKA MAENEO
MBALIMBALI YA WILAYA YA ILEMELA MKOANI MWANZA, ASKARI WALIFANYA DORIA
PAMOJA NA MISAKO KATIKA MITAA MBALIMBALI YA WILAYA TAJWA HAPO JUU NA
KUFANIKIWA KUWAKATA WATU WA NNE WAKITUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA
HARAMU YA BHANGI PAMOJA NA POMBE AINA YA GONGO KITENDO AMBACHO NI
UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI
WATUHUMIWA
WALIOKAMATWA 1.JANETH MASOLE MIAKA [30], MKAZI WA KISEKE ALIYEKAMATWA
AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 83, 2. SUZANA DOTTO MIAKA [50], MKAZI WA IGOMBE
ALIYEKAMTWA AKIWA NA POMBE YA GONGO LITA 60, 3. MADURU MATHIAS MIAKA
[35], MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMATWA AKIWA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA
POMBE YA GONGO NA, 4. BUSHESHE FAIDA MIAKA [20], PIA MKAZI WA IGOMBE
ALIYEKAMATWA NA BHANGI MISOKOTO MIWILI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA
SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA
WATUHUMIWA WOTE WA NNE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU
MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZA UHALIFU WANAOJIHUSISHA NAO YAKIENDELEA,
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA
UHALIFU ZINAZO WAKABILI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
MSANGI ANAWATAKA WANANCHI WAENDELEE KUTULIA LAKINI WAKIENDELEA KUTO
USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLSI ILI LIWEZE KUFANYA KAZI VIZURI NA
KUTOKOMEZA UHALIFU WA AINA ZOTE KATIKA MKOA WA MWANZA.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
0 comments:
Post a Comment