Mkanda (kulia) akimwonesha msomaji wa Amani, Issa Hamad, sehemu yenye kuponi ya bahati nasibu.Hamadi akijaza kuponi yake. Mkanda (kulia) akimfafanulia jambo msomaji wa gazeti la Amani namna ya kushiriki bahati nasibu hiyo.John Helbert mkazi wa Kunduchi Dar akijaza kuponi.Msomaji wa gazeti la Amani mkazi wa Kunduchi Dar ambaye jina lake halikujulikana (kulia) akijaza kuponi.Mkanda (kushoto) akimsaidia msomaji kukata kuponi baada ya kumaliza kuijaza.
NI hatua za mwisho za
lala-salama ambapo zimebaki siku 12 kuchezeshwa droo kubwa ya bahati
nasibu ya ‘Shinda Nyumba’ na jana Alhamisi promosheni ya shindano
hilo inayoendelea iliwafikia wakazi wa Kunduchi, Dar, waliojitokeza
kwenye gari la matangazo kuchangamkia gazeti la Amani na kushiriki
kujaza kuponi za bahati nasibu.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na
Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi,
Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Maofisa masoko wa Global
Publishers,Yohana Mkanda na Jimmy Haroub waliwafikia wasomaji katika
mitaa mbalimbali ya maeneo ya Kunduchi na kuwahamasisha kushiriki bahati
nasibu hiyo.
Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda
alirudia wito wake kwamba: “Siku zimebaki 12 nunueni magazeti ya Global
mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani
unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Kazi
kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”
Naye Meneja Mkuu wa Global Publishers
Ltd, Abdallah Mrisho, juzi Jumatano akizungumza na wanahabari baada ya
kutembelea nyumba hiyo eneo ilipo kwa ajili ya kuona mandhari na samani
zilizomo ndani ya nyumba hiyo iliyoko Salasala alisema:
“Nyumba hiyo iko tayari kukabidhiwa mshindi atakayepatikana katika
droo inayotarajiwa kufanyika Juni 30 mwaka huu kwenye viwanja vya
Mbagala- Zakhem jijini Dar,”
0 comments:
Post a Comment