POLISI
mkoani Tanga imewaua watu watatu katika mapigano ya risasi wanaodaiwa
kuhusika katika mauaji ya watu jijini humo wakiwamo watu wanane
waliochinjwa katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima.
Limewahakikishia
wananchi kwamba eneo la Amboni yakiwemo Mapango ya Majimoto yanayodaiwa
kutumiwa na wahalifu waliosababisha mauaji hasa ya wakazi wanane wa
Kibatini lipo salama, baada ya watuhumiwa wengine watatu na silaha
mbalimbali kukamatwa juzi.
Waliokamatwa
ni Abdulkarim Singano, Seif Jumanne na Ramadhani Mohamed ambao baadaye
walikufa kutokana na majeraha ya risasi wakati wa mapigano katika msitu
wa Kibatini wakati askari wakijaribu kuwadhibiti, siku moja baada ya
Abuu Seif anayedaiwa kuwa kiongozi wao kuuawa jijini Dar es Salaam.
Silaha
zilizokamatwa ni bunduki mbili aina ya SMG, bastola moja, risasi 30,
mapanga, majambia ambavyo vimepatikana kupitia msako ulioshirikisha
kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi na usalama vilivyohusisha askari
kutoka majeshi yote.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo alibainisha hayo wakati akitoa
taarifa ofisini kwake jana kwamba, wahalifu hao walikamatwa Juni 28,
mwaka huu wakati askari walipokuwa katika harakati za kuwakamata kwenye
msitu wa Kibatini jirani na mapango ya Majimoto, Kata ya Mzizima jijini
Tanga.
“Majambazi
waliohusika kuua wananchi wanane pale Kibatini ndio tumewakamata lakini
kwa bahati mbaya watatu kati yao wamekufa wakati wakidhibitiwa na
askari,” alisema Kamanda Paulo.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na imedhibitiwa.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na imedhibitiwa.
Mapema
wiki hii, Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, walitangaza kumuua
Abuu Seif aliyeshiriki katika mauaji ya Tanga, baada ya kumpiga risasi
alipokataa kujisalimisha baada ya kubainika kujificha katika nyumba moja
jijini Dar es Salaam. Alifariki dunia akipelekwa hospitali.
0 comments:
Post a Comment