Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe amekamilisha ziara ya
siku nne Singida, Tabora, Shinyanga na Geita ambapo amefanya mkutano wa
hadhara katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na
Buseresere mkoani Geita.
akizungumza
katika mkutano huo Rais Magufuli amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi
ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha
zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo
la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Katika
agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya
udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi
kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali
itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
>>>’Ninafahamu
mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo,
wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika
shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi
waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina
wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za
wanafunzi laki moja wagawane’
>>>’Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali’
0 comments:
Post a Comment