August 17 2016 kuelekea kuanza
msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar es Salaam
ulichezwa mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa
2015/2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans na mshindi wa pili wa
Ligi Kuu Azam FC hiyo ikiwa ishara ya kukaribia kuanza kwa msimu mpya wa
Ligi.
Katika mchezo huo ambao dakika 45 za
kwanza zilikuwa zinaonesha kuna kila dalili ya Yanga kuondoka na Ubingwa
wa Ngao ya Hisani, umemalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa
mikwaju ya penati 4-1, hiyo inatokana na mchezo huo kumalizika kwa sare
ya goli 2-2.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri kwa
Yanga baada ya dakika ya 20 Donald Ngoma kupachika goli la kwanza kwa
mkwaju wa penati na dakika 2 baadae kuongeza goli la pili kwa kutumia
vyema pasi ya Amissi Tambwe, kipindi cha pili ndio Yanga waliendelea
kumiliki mpira na kila mtu akiamini mchezo utamalizika hivyo.
Dakika ya 74 Azam FCwalipata goli
kupitia kwa Shomari Kapombe lakini kujisahau kwa Yanga walijikuta
wakisababisha penati na John Bocco akaisawazishia Azam FC katika dakika
za nyongeza, kwa upande wa mikwaju ya penati zilipigwa na John Bocco,
Shomari Kapombe, Himid Mao na Kipre Bolou wakati za Yanga zilipigwa na
Deogratus Munish huku Haruna Niyonzima na Hassan Kessy walikosa.
GOAL AND HIGHLIGHTS: Yanga vs MO Bejaia August 13 2016, Full Time 1-0
0 comments:
Post a Comment