Wednesday, 13 February 2019

Picha: BALOZI IDD AUNGURUMA SHINYANGA MJINI..AWATAKA WANA CCM KUACHANA NA SIASA ZA MAKUNDI

...


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga amehutubia mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye ni Makamu wa Rais Bunge la Afrika.

Mkutano huo ambao ni sehemu ya kusherekea miaka 42 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi umefanyika leo Jumatano Februari 13,2019 katika Viwanja vya Zimamoto vilivyopo Mjini Shinyanga.

Akihutubia mkutano huo amewataka wanaCCM kuwa na umoja,kushirikiana na kuacha siasa makundi kwani makundi yanagawa chama.

“Tushirikiane,tushikamane ili chama chetu kiwe imara na tuweze kushinda kwenye uchaguzi,nawasihi muache siasa za makundi”,amesema Balozi Idd.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

PICHA NYINGI ZAIDI ZINAKUJA HIVI PUNDE
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger