WABUNGE
wameonesha wasiwasi kuhusu kupunguzwa kwa fungu la fedha katika Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na kuonya kuwa huenda hatua
hiyo ikampunguzia Rais John Magufuli kasi ya utumbuaji majipu,
anayoifanya kwa wabadhirifu wa fedha za umma au kuua kabisa utaratibu
huo.
Wabunge
hao walionesha wasiwasi huo kwa nyakati tofauti bungeni mjini hapa
Dodoma, wakati wakichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa
fedha 2O16/17 inayoanza kutekelezwa Julai mosi, mwaka huu.
Miongoni
mwa wabunge hao ni wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), aliyeeleza kuwa,
kupunguza fedha katika ofisi hiyo ni kumkwamisha Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya kazi yake kwa ufanisi na tija.
Kwa
mujibu wake, kumkwamisha huko pia ni dalili ya kuukumbatia ufisadi kwa
sababu ofisi hiyo ya CAG ndio inayofanya kazi ngumu na kubwa ya
kuwafichua mafisadi nchini, hivyo inahitaji kujitosheleza kibajeti na
kuepuka kuhitaji msaada kutoka kokote kwingine.
“Kitendo
cha kuminya fungu la ofisi ya CAG kwa kupunguza kiasi cha fedha
inachopewa kutoka shilingi bilioni 74 kwa mwaka wa fedha unaoisha hadi
shilingi bilioni 44 kwa mwaka mpya wa fedha unaoanzia Julai Mosi, ni
kuifanya ofisi hiyo ishindwe kuyabaini majipu (wabadhirifu, mafisadi),” Lugola alisema.
0 comments:
Post a Comment