POLISI
mkoani Mwanza imemuua jambazi baada ya mtu huyo akiwa na wenzake wawili
kurushiana risasi na polisi waliokuwa doria baada ya kushindwa kutii
amri ya kusimama walipotakiwa kufanya hivyo na polisi.
Akizungumza
ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
alisema mauaji hayo yalitokea Mei 31, mwaka huu saa 4.10 usiku katika
Mtaa wa Ilemela katikati ya barabara inayopita kati ya eneo zilipo
ofisini za Radio Free Afrika (RFA) na Kiwanda cha Samaki cha Mwanza.
Alisema
polisi waliokuwa doria katika eneo hilo waliwatilia mashaka watu watatu
waliokutana nao usiku huo wakiwa wamebeba sanduku na walipoamriwa
kusimama, hawakutii.
“Hawakutii,
badala yake watu wale waliongeza mwendo, huku mmoja wao akitoa mfuko
uliokuwa na kitu, kumbe ilikuwa ni bunduki na kuanza kurushiana risasi
na polisi,” alieleza Kamanda Msangi.
Alisema
mtu huyo alifyatua risasi kati ya tatu hadi nne kwa polisi, lakini
hazikuleta madhara kwa walinzi hao wa usalama wa raia waliomuua kujibu
mapigo kwa kumpiga risasi na kumuua papo hapo huku wenzake wawili
wakikimbia na kuelekea kusikojulikana.
Alisema
baada ya tukio hilo, polisi walimkuta jambazi huyo akiwa na silaha aina
ya SMG iliyochakaa na namba zake zikiwa zimefutika ikiwa na magazini
yenye risasi 16. Alisema upelelezi kwa ajili ya tukio hilo unaendelea.
Kamanda
Msangi alisema silaha iliyokamatwa hutumika kwenye majeshi na kuwa
mwananchi wa kawaida haruhusiwi kutumia silaha ya aina hiyo.
“Tutapeleka silaha hii kwa wataalamu kwa ajili ya kuitambua maana bunduki ya aina hii hatuna kwenye majeshi yetu,” alisema na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya utambuzi.
0 comments:
Post a Comment