MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wanaCCM
kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha chama na kuahidi kuyatumbua majipu
hadi katika chama.
Dk
Shein alisema kwa upande wa serikali kazi ya kuunda serikali inaendelea
na kuwataka watendaji walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kufanya
kazi kwa maslahi ya taifa na wananchi wake.
Alisema
mtendaji atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake katika sehemu za kazi
ni bora akajiondoa kabisa hata kabla ya kusubiri kuondolewa.
Kwa
upande wa CCM, aliwataka watendaji kusimamia majukumu yao bila ya
kusubiri kusimamiwa kwa ajili ya kuimarisha chama, kwani kazi hiyo ni ya
kujitolea na waliopewa dhamana hizo wanatakiwa kulifahamu hilo na
kujituma kwa kujenga chama imara.
“Wapo watendaji katika chama hawatekelezi na kusimamia majukumu yao vizuri na kama ndiyo majipu yenyewe basi tutayaondoa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment