Wednesday, 31 August 2016
MTANDAO WA WANAFUNZI (TSNP) MKOA WA KIGOMA WATEMBELEA SHULE MBALIMBALI ZA MJINI KIGOMA
Mr. Abdul Nondo, ni mratibu wa mtandao wa wanafunzi TANZANIA (TSNP) mkoa wa kigoma. Kuna program ameianzisha ya kuzungukia Shule mbali mbali TANZANIA,
Mr. Abdul Nondo |
kuhamasisha wanafunzi kidato cha 1 hadi cha nne kutimiza wajibu wao, na kuvaa majukumu Yao, na kujifungia Kwa Muda kutekeleza majukumu Yao, kuwa na nidhamu, kujitambua nini wanapaswa kufanya,kuepuka makundi ambayo hayana utaratibu wa kitaaluma,kupanga ratiba yao ya kujisomea, changamoto wanafunzi wengi hawana utaratibu wa kujisomea, wazazi wao mkoa wa kigoma hawana utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Wanafunzi wengi wapo huru saana kufanya mambo ambayo si ya msingi Kwa Muda huu wakiwa shuleni, ametembelea Shule ya RUBUGA na kirugu sekondari kigoma, wanafunzi wamekiri hayo na wameahidi kubadilika kuanzia leo hii,, hii Ndio kazi ambayo mtandao wa wanafunzi (TSNP), tunayoifanya. Mtandao tumeunda TSNP CLUBS, ili tuendelee kupata taarifa kutoka Shule hizo. Bado tunaendelea na kazi hiyo, baada ya kigoma ni mikoa mingine.
Pia anapenda kushukuru afisa elimu sekondari manispaa ya kigoma ujiji, ndug,
Emmanuel L. Kitemi Kwa ushirikiano wake, pia napenda kumpongeza na
kumshukuru meya wa manispaa ya kigoma ujiji,ndug, hussein Ruvagwa, Kwa
sapoti yake kubwa na kutambua umuhimu wa elimu mkoa wa kigoma, mimi ni
Abdul Nondo mratibu wa mtandao wa wanafunzi TANZANIA (TSNP) mkoa wa
kigoma, na mjumbe wa idara ya haki na wajibu wa wanafunzi. No 0762
599672, page sauti ya wanafunzi Tanzania
MBOWE ATANGAZA KUSITISHA MAANDAMANO YA OPARESHENI UKUTA SEPT 1
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo,Freeman Mbowe
ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA yaliyokuwa
yamepangwa kufanyika kesho nchi nzima hadi tarehe moja Octoba.
Akizungumza na wanahabari leo, makao makuu ya chama hicho, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema, Chadema inalazimika kuahirisha maandamano na mikutano ya kesho kutokana na kuheshimu wito wa viongozi wa dini zote waliowaomba.
“Viongozi wa dini zote hapa nchini kuanzia, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania, Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), Katibu Mkuu wa Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Mufti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) na Mufti Mkuu wa Zanzibar, wametusihi tuahirishe ili wao wazungumze na Rais John Magufuli kutafutia suluhu suala hili,” amesema Mbowe.
Mbowe amezitaja taasisi na watu wengine wenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi waliokiomba chama hicho kuahirisha maandamano na mikutano hiyo kuwa ni Mzee Joseph Butiku ambaye ni Mwenyekiti wa Tasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mama Maria Nyerere ambaye alizungumza na Edward Lowassa kwa niaba ya chama hicho.
“Kwa heshima ya viongozi wetu wa dini na taasisi hizi, tunawatangazia wanachama wetu kote nchini kuwa tunaahirisha maandamano hayo kwa muda wa mwezi mmoja ili kuwapa nafasi viongozi hawa waonane na Rais Magufuli na kama asipowaelewa hata hao, sisi tusilaumiwe,” amesisitiza Mbowe.
Msikilize hapa chini akiongea

Tuesday, 30 August 2016
Walimu 22 Azania Sekondari Waondolewa Baada ya Shule Kuwa ya Mwisho Matokeo Kidato cha Sita
Walimu
22 wa Shule ya Sekondari ya Azania Manispaa ya Ilala, akiwamo Mwalimu
Mkuu, wamehamishwa kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na matokeo mabaya
ya kidato cha sita.
Taarifa hizo ziliongeza kuwa kati ya walimu 17, wengi wao walikuwa wanafundisha mchepuo wa ECA ambao wote wamehamishwa na kupangiwa shule nyingine huku wengine wakihamishiwa shule za kata na kupangiwa kufundisha kidato cha kwanza, pili na tatu. Awali, walimu hao walikuwa wakifundisha kidato cha tano na sita.
Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo ya kidato cha sita na shule hiyo kongwe ikajikuta imo katika kundi la shule 10 za mwisho zilizokuwa na matokeo mabaya.
Aliyedaiwa kuuawa na polisi azikwa saa 4.00 usiku
Mwili wa marehemu
Stanslausi Kalinga (42) aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi ulizikwa
saa 4.00 za usiku nje kidogo ya Mji wa Mlowo baada ya ndugu zake
kukubali yaishe.
Marehemu
ambaye ameacha mke na watoto wanne alifariki akiwa mikononi mwa polisi
jambo lililosababisha vurugu kutoka kwa wananchi ambao walitaka mwili
uzikwe na polisi wenyewe.
Wananchi
hao walisusia mwili tangu Agosti 27 hadi juzi usiku ambapo mwili
ulirudishwa kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya ulikopelekwa kwa uchunguzi
kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ernest Paringo.
Hata hivyo hakuna majibu ya uchunguzi yaliyotolewa licha ya ndugu wa marehemu kushiriki katika kuufanyia uchunguzi mwili huo.
Tahadhari dhidi ya Taarifa za uongo kuhusu kutangazwa kwa Orodha ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2016/2017
Tahadhari dhidi ya Taarifa za uongo kuhusu kutangazwa kwa Orodha ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2016/2017
Wanafunzi hewa 4,445 wabainika Kahama
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo, amesema Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ina wanafunzi hewa 4445 ambao wanasoma katika shule za sekondari za serikali kinyume na utaratibu.
Jaffo aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri za Msalala na Mji, juzi, katika ziara ya kushitukiza, ambapo aliwaasa kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu za kuwahudumia wananchi.
Alisema kuwepo kwa idadi hiyo kubwa ya wanafunzi hewa katika shule za sekondari kunatokana na maofisa elimu kutokujua takwimu za wanafunzi na kuongeza kuwa, muda mwingi wamekuwa wakikaa ofisini bila ya kutembelea maeneo ya kazi.
Naibu Waziri huyo alisema, takwimu za utengenezaji wa madawati, zimekuwa kinyume na ilivyotarajiwa, hali ambayo imesababisha kuchelewa kumalizika kama iliovyokuwa imepangwa na Rais John Magufuli.
Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri huyo aliwaonya watumishi hao kutotumia fedha vibaya zitakazotolewa na wizara hiyo, kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya barabara katika halmashauri ya mji wa Kahama.
Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Halmashauri ya Mji wa Kahama, ina changamoto nyingi zikiwamo za miundombinu ya barabara, kuzidiwa kwa wagonjwa wanaotoka katika wilaya 16 katika hospitali ya halmashauri ya mji pamoja na upungufu wa watumishi.
Alisema Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, imezidiwa na wagonjwa ambao wanatoka katika sehemu mbalimbali zilizopo jirani, hali ambayo watumishi wake wanapata wakati mgumu katika kutoa huduma na wakati mwingine kushindwa kutoa huduma kwa wakati.
Lipumba Aendelea Kung'ang'ania Uenyekiti Wake CUF
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti
cha uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana
visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama,
hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa
ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.
“Kikao
hicho hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu linakaa halafu Naibu
Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna wajumbe wengine
hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba
Lipumba
aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua
kuandika barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na
sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho.
“Nilimuandikia
barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema anasubiri ushauri wa
kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha kuwa sasa mimi
naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof Lipumba.
Aidha aliongeza kuwa alitaka kujieleza katika mkutano mkuu mbele ya wanachama, lakini mkutano ule ukavurugwa.
Kuhusu
kuwepo kwa tofauti kati yake na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif
Sharif Hamad, Prof Lipumba amesema kuwa huenda kuna tofauti kwa kuwa
mara nyingi huwa hamuelewi jinsi anavyokiendesha chama bila kifuata
misingi ya kidemokrasia.
“Katibu
Mkuu anamdharau na hampi heshima yake Naibu Katibu Mkuu Bara, mara
nyingi huamua mambo yake bila kushirikisha viongozi wengine, halafu sasa
anataka kufukuza wanachama, huwezi kuwa na chama halafu ufukuze
wanachama, wanachama wanatafutwa duniani kote, halafu wewe unawafukuza,
hizo ni dalili za uongozi wa kiimla, kuongoza chama unapaswa kujali
demokrasia na siyo kuwa dikteta ndani ya chama” Amesema
Kuhusu
Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi, Lipumba
amesema kuwa hatambui maamuzi hayo, na wala hamtambui Mtatiro kama
kiongozi wa chama hicho bali mjumbe wa Mkutano Mkuu, nafasi ambayo yeye
ndiye aliyempa.
“Mtatiro
hawezi kuwa mwenyekiti, mimi ndiye mwenyekiti wa chama, Mtatiro
alishindwa hata kuongoza mkutano mkuu, ukavurugika, hawezi, simtambui”