Tuesday, 10 June 2014

YAWALIMWENGU:MJAE AWEKEWA MTI SEHEMU ZAKE ZA SIRI

...
MJANE mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za maadili) (24) mkazi wa Kijiji cha Omuga, Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara amefanyiwa ukatili wa kutisha wa kusimikwa kijiti sehemu zake za siri na shemeji zake ili kulazimishwa kuhama baada ya mumewe kufariki dunia.

Msichana anayedaiwa kufanyiwa ukatili wa kutisha wa kusimikwa mti sehemu zake za siri na shemeji zake ili kulazimishwa kuhama baada ya mumewe kufariki dunia akionyesha mti uliohusika kwenye tukio hilo
WANANCHI zaidi ya 500 wa Kijiji cha Moivaro na Chekereni katika Kata ya Moshono, wilayani Arumeru
Baba mzazi wa mjane huyo,  Alex Allal aliliambia  gazeti hili kuwa mara baada ya kupata taarifa za ukatili huo aliofanyiwa mwanaye aligundua tayari alishatimuliwa kwake akawa anatangatanga na mtoto wake mdogo wa kiume mwenye miaka saba.
Baba huyo alidai amefedheheshwa na kitendo cha shemeji wa binti yake kwa kumpiga kisha kumfanyia ukatili huo.
“Baada ya kufanyiwa unyama huo, tuliripoti polisi na kupewa RB namba UTE/RB/256/2014 na mmoja wa shemeji zake aitwaye Isaya Elphas alikamatwa Mei 28, mwa huu na wengine kutoweka,” alisema.
Naye mjane huyo alidai kuwa, alianza
kunyanyaswa na shemeji zake hao baada ya mume wake Samwel Elphas kufariki dunia mwaka 2012.
Aliyataja manyanyaso aliyoyapata ni pamoja na kudaiwa kuporwa ardhi ekari mbili zilizokuwa na mashamba ya miwa, migomba,
mihogo na mahindi alizoachiwa na marehemu mumewe.
Alidai familia ya wakwe zake imemuomba aondoe shauri hilo katika vyombo vya dola ili wajadiliane na kupata suluhu.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger