Tuesday 29 April 2014

UNGA WAZIDI KUMTESA RAY C

...

Rehema Chalamila ‘Ray C’ katika pozi.
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye aliwahi kuathirika na utumiaji wa ‘unga’, hivi karibuni alitinga ofisi ya kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya na kuomba kupatiwa majina, idadi na sehemu walipo watumiaji wa mihadarati hiyo ili aweze kuwasaidia kwa kuwapa somo, kitu kinachotafsiriwa kama bado unamtesa.
Ray C katika harakati zake akifanya mahojiano na msanii wa Hip hop, ambaye yupo mbioni kuachana na madawa ya kulevya, Ibra the Hustler.
Ray C anadaiwa kufika katika ofisi hizo, Aprili Mosi, mwaka huu, saa nne asubuhi hali iliyozua gumzo kwa askari waliomuona ambao walijiuliza kitu alichokifuata.
Akizungumza na Uwazi, kamanda wa kitengo hicho cha madawa ya kulevya, Godfrey Nzowa alikiri kufika kwa msanii huyo ofisini kwake na kutoa madai hayo lakini alimwelekeza kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani huko kuna kitengo kinachoshughulika na watu wenye matatizo ya akili wakiwemo watumiaji wa madawa ya kulevya.
Ray C.
Kamanda huyo alionesha kufurahishwa na kitendo cha msanii huyo ambaye pia anamiliki taasisi yake yenye lengo la kuwasaidia waathirika wa matumizi ya madawa hayo kwa kuwapa elimu, akisema atatoa msaada mkubwa kwa wenzake.
Aliwataka watumiaji wa madawa hayo ambao wameshindwa kuacha, wamfuate msanii huyo ili awape elimu na amewaonya wote wanaotumia na kusafirisha madawa hayo.
“Wote wanaotumia na kuuza madawa hayo waache mara moja kwani kikosi kazi kinachopambana na biashara hiyo kimejipanga kila kona ili kukomesha biashara hiyo haramu,” alisema Kamanda Nzowa
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger