Wednesday, 23 April 2014

NISHA: SIJAWAHI KUCHUKULIWA NA PEDESHEE

...
SALMA Jabu maarufu kama Nisha, ni mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri katika kiwanda cha filamu Tanzania. Amefanya kazi nyingi zinazomfanya kuwa mmoja wa mastaa wanaoongoza kwa kushiriki katika movie nyingi.
Salma Jabu 'Nisha'.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta na kufanya naye mahojiano maalum kuhusu mambo mbalimbali yanayohusiana na sanaa yake.
Risasi: Mambo vipi Nisha?
Nisha: Poa kabisa, niambie
Risasi: Unaizungumziaje sanaa yako kwa ujumla wake?
Nisha: Sanaa yangu ni safari ndefu sana na naamini ndiyo kwanza nipo robo yake.
Kuna mambo mengi magumu, mojawapo ni kupata vikwazo vya hapa na pale, pia wapo baadhi yetu wanapata labda skendo, badala ya kuwahukumu wenyewe, lakini tunachukuliwa kuwa wote ndivyo tulivyo jambo ambalo siyo kweli.
Mtu unatamani kuwa fulani, lakini unawekewa vikwazo kwa sababu tu ya ule msemo wa samaki mmoja akioza, basi wote wameoza.
Risasi: Vipi kuhusu soko la bidhaa zetu?
Nisha: Soko ni zuri sana, ni kujua tu mashabiki wako wanapenda nini basi.
Risasi: Unadaiwa wewe una fedha sana, kuna mtu yuko nyuma yako?
Nisha: Sina mtu nyuma yangu, pesa ni juhudi zako mwenyewe, kikubwa nafanya kazi kwa bidii, napenda sana kazi yangu, alhamdulilah sasa nimekuwa na kampuni yangu mwenyewe ya kuandaa filamu (Nisha’s film production).
Nisha katika pozi.
Kwa mfano nimeandaa filamu kama Tikisa, Pusi na Paku, Kashfa na Gumzo na zingine. Hiyo ndiyo siri ya hizo pesa wanazozitaja, napenda kuweka akiba kwa kufungua mradi, saluni yangu na duka la samani, ndiyo vinaendesha maisha ya kawaida ya nyumbani.
Risasi: Umri unaenda, vipi umeolewa?
Nisha: Nina mtu alhamdulilah, Inshaalah niombeeni dua, sijawahi sumbuliwa kwani mimi mapema nimeanza kujiajiri mwenyewe.
Risasi: Umejaaliwa kupata mtoto?
Nisha: Sina watoto ila napenda watoto, kila mtoto ni wangu inshaallah nataka kuanzisha familia, nasubiri Mwenyezi Mungu ajibu kwani kila kitu kimeandikwa na yeye, mimi siwezi jua lini, saa na wapi.
Risasi: Kuna maneno juu ya wasanii kujirahisisha kwa watu wenye fedha, wanaoitwa mapedeshee, unazungumziaje?
Nisha: Mimi sijawahi kuwa na pedeshee wala simuhitaji, nakuwa na mtu kwa mapenzi ya kweli, awe maskini au tajiri ilimradi moyo wangu umempenda, kikubwa tabia na maelewano na anipende kwa dhati.
Risasi: Unafikiri kwa nini baadhi ya wasanii na wasichana wengine wanaamua kujiuza?
Nisha: Wengine wanashindwa kujiajiri kwa kukosa mtaji (kwa wasiokuwa nao nawaombea wapate) wanaojiuza ni tamaa,
kutojitambua na kukosa malengo, mimi nina malengo na siku moja niwe mfano kama Oprah Winfrey na kadhalika, sijaridhika kwa nikipatacho, nafanya kazi kwa bidii ili kupata zaidi Inshaalah.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger