Umoja
wa Mataifa unasema kuwa vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan
Kusini viliwaua mamia ya watu kwa sababu ya kabila lao wakati
vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika
hilo, watu hao walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa
wanahifadhiwa kama vile msikitini, makanisani na hospitalini.Umoja
huo umesema kuwa watangazji katika baadhi ya vituo vya redio walitumia
lugha ya chuki na uchochezi na kuwataka watu wa kabila fulani kuondoka
mjini humo huku wakiwashauri wanaume kuwabaka wanawake.
0 comments:
Post a Comment