Mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo
mjini Shinyanga ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akifanya jaribio la
kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 katika eneo la Ngokolo
mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema kuwa tukio
hilo limetokea Aprili 20 ,mwaka huu saa tisa usiku.
Amesema
siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke
huyo na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika
kujihami kwake ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu kichwani ,akafariki
dunia akiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi.
0 comments:
Post a Comment