Wednesday 30 April 2014

Chipukizi Mtanzania kwenda Barcelona

...


Nick Van Lawick (13 , ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota.
Siku zote katika maisha ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuheshimu ndoto zetu hata kama tunadhani ni ndoto ndogo. Kuziheshimu ndoto zetu na kuzitimiza, kunahitaji nidhamu ya ziada, ingawa wapo wanaozifikia andoto zao kwa bahati.
Wengi husema wanataka kutimiza ndoto zao, lakini ni wachache hufanikiwa kutimiza ndoto zao. Hata hivyo kwa kuwa binadamu tuna ndoto tofauti tofauti ni ngumu kuwa na kanuni moja ya jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Mtoto Nick Van Lawick (13), anayesoma shule ya kimataifa ya Dar es Salaam Independence School, ana ndoto ya kuichezea klabu ya Barcelona ya Hispania na anatarajia atatimiza ndoto hiyo.
Hiyo inatokana na kipaji alichonacho cha soka na mipango iliyofanywa na wazazi wake, ambao watamkutanisha Nick na mtaalamu wa viungo wa klabu ya Barcelona, Juanjo Brau.
Baba mzazi wa Nick anayeitwa Hugo van Lawick anasema: “Nick amepata nafasi ya kwenda kupewa mafunzo na Brau.
“Mama yangu Jane Goodall ni rafiki wa karibu wa Brau na mama yangu anafahamu kipaji cha mpira cha mjukuu wake, ndio maana aliona awasiliane na rafiki yake kuangalia nafasi ambayo Nick anaweza kujiendeleza zaidi kisoka.
“Brau alishauri kuwa Nick aanze kwa kumpa mafunzo ndipo mchakato wa kumtafutia nafasi katika timu ya vijana ya Barcelona ufanyike.”
Kwa upande wake Nick, anayesoma kidato cha pili, anasema anapenda sana mpira na muda wake mwingi huutumia katika mambo yahusuyo mpira huku akiipenda zaidi klabu ya Barcelona kwa sababu ya staili yao ya uchezaji.
Aota kuisaidia Tanzania
Nick (pichani), ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota, atatumia sehemu ya fedha atakazopata kusaidia mambo mbalimbali nchini, hasa hasa tatizo la umeme na kusaidia watoto walio kwenye mazingira magumu. (CHANZO: MWANANCHI) (FS)

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger