Tuesday 22 April 2014

Kikwete Ateua Mabalozi Wapya; Hakuna Mzanzibari

...

Wakati Wazanzibari wanaendelea kulilia haki yao ndani ya Muungano, na hatua za kutafuta katiba mpya ndio inaendelea Dodoma (CCM watupu waliobaki), juzi tu, rais Kikwete ameteua mabalozi wapya lakini hakuweza kumchagua hata Mzanzibari mmoja. Hivi kweli hakuna mzanzibari hata mmoja anayefaa kuwa balozi au angalau kaimu?

Najua kuwa Balozi Mohammed Mwinyi Mzale ni Mzanzibari na mmoja ya mabalozi waliostaafu. Alikuwa anawakilisha TZ kule Sweden. Sasa ilikuwa vizuri kama angalau mbadala wake ukwe kwa Mzanzibari vile vile, si lazima awe balozi wa Sweden bali popote pale hata Sudan ya Kusini au Nigeria.
Hivi balozi kama yule mama pale Washington DC, balozi Mula Mula anafanya nini pale, au ana sifa gani za ziada wengine hawana? Hata sio ‘attractive’ kama sifa za mabalozi zinazotakiwa. Yuko very shabby, na hata mavazi yake kama vile yuko kwao kijijini Bukoba.
Inasikitisha sana sana kuona utengano huu, ubaguzi na dharau hii kwa Zanzibar na Wazanzibari.
JK endelea kutupiga bao!Kesho mteuwe Ridhwan Kikwete kuwa Waziri na baadaye Rais wetu wa Zanzibar.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger