Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga akizungumza juu ya mipango ya dharula itakayo fanywa ili kuokoa janga hilo. |
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo Dr Victory Kanama akizungumza juu ya tukio hilo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Bweni
Moja la Wavulana lenye vyumba zaidi ya Sita katika shule ya
Sekondari ya Ivumwe inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa
moto.
Tukio
hilo limetokea leo April 23 majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya
wakati wanafunzi hao wakiwa madarsani kuendelea na masomo yao kama
kawaida.
Akizungumza
katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari
Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi
wakati teyari wanafunzi wakiwa madarasani.
Amesema
taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi
waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo
yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo.
Amesema
mara baada ya kupata habari hizo walitoa taarifa kwa kikosi cha
zimamoto ambacho kilifika mara moja na kuanza juhudi za kuuzima moto
huo.
Amesema
pamoja na kikosi hicho cha zimamoto kufika shuleni hapo mapema na
kuzima moto huo lakini teyari moto huo ulikwisha teketeza asilimian
kuwabwa ya mali zilizomo katika mabwani hayo.
Amesema
kwa kiwango kikubwa vitu vingi vimeteketea kwa moto huo hususani
vitanda na magodoro ambayo ndiyo yaliyoungua vibaya pamoja na vitu
vingine vya wanafunzi hao.
Aidha
kwa mujibu wa Dakta Kanama hakuna mwanafunzi yoyote aliye poteza maisha
kutokana tukio hilo licha ya mmoja wa wanafunzi kujeruhiwa mkononi na
kitu kinacho dhaniwa kuwa ni kioo katika harakati za kuokoa vitu ambapo
teyari amekwisha fikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Aidha
kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi
CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga amesema mabweni hayo yalichukua
jumla ya wanafunzi 160 ambao ni wavulana huku chanzo cha moto huo
kikiwa bado bado hakijajulikana.
Amesema
kwa sasa juhudi zinazofanyika na Chama kwa kushirikiana na uongozi wa
shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwahifadhi wanafunzi
hao.
Amesema litatengwa darasa moja kwa muda ambalo litatumika kama bweni wakati wakiendela kufanya utaratibu mwingine.
0 comments:
Post a Comment