Monday 21 April 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 2014/2015

...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679 Faksi: 022-2113271 Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO MAALUMU YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA
STASHAHADA KWA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KWA MWAKA WA MASOMO
2014/2015
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, anatangaza nafasi za Mafunzo Maalumu ya
Ualimu Tarajali Ngazi ya Stashahada kwa masomo ya Sayansi na Hisabati. Lengo la mafunzo
haya ni kuwajengea uwezo washiriki katika taaluma ya masomo mawili ya kufundishia katika
shule za Sekondari. Mafunzo haya yatafanyika kwa utaratibu ufuatao:
(i) Watakaochaguliwa watapatiwa mafunzo ya miezi mitatu ili kuimarisha taaluma ya masomo
ya Sayansi na Hisabati waliyosoma katika Kidato cha Tano na cha Sita. Mwisho wa
mafunzo haya, washiriki watafanya Mtihani Maalumu kwa lengo la kutathmini uwezo wao
(competence) katika masomo tajwa.
(ii) Watakaofaulu Mtihani wa mafunzo haya watajiunga na mafunzo ya ualimu ya kawaida
Ngazi ya Stashahada kwa miaka miwili kuanzia mwezi Julai 2014.
SIFA ZA WAOMBAJI
Waombaji wawe wamehitimu Kidato cha Sita kati ya mwaka 1998 na 2013 na kufaulu kwa
kiwango kisichopungua ‘Subsidiary pass’ mbili katika tahasusi za PCB, PCM, PGM, CBG, CBA
na CBN.
MAELEKEZO MUHIMU
(i) Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume maombi ofisi za Maafisaelimu wa Mikoa au
Wilaya; au watume maombi yao kwa njia ya posta yakionesha anuani zao (za posta, au
anuani ya barua pepe na simu); pamoja na nakala za vyeti vya ufaulu wa Kidato cha 4 na
cha 6;
(ii) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo haya yatatolewa kwenye Tovuti ya
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz; OWM-TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz; na katika mbao za matangazo Wizarani, ofisi za Maafisaelimu wa
Mikoa na Wilaya;
(iii) Barua za kujiunga na mafunzo kwa watakaochaguliwa zitatolewa na vyuo
watakavyopangwa kwa kutumia anuani zao; na
(iv) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi:
www.moe.go.tz; OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na kwenye mbao za matangazo
Wizarani, Maafisaelimu wa Mikoa au Wilaya; na Vyuo vya Ualimu.
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Idara ya Elimu ya Ualimu)
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 28/02/2014.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger