Monday, 21 April 2014

SHAMSA FORD AONGOZA KUKATA NYONGA MACHOZI BENDI

...


Staa wa bongo Muvi, Shamsa Ford.
Kama kawa ni Ijumaa nyingine ambayo mapaparazi wetu, Musa Mateja ‘Toz’, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100, zamani Mzee wa Mapikipiki’, Dustan Shekidele ‘Mzee wa Mji Kasoro Bahari’, Shakoor Jongo ‘Zungu Fedha,’ Haruni Sanchawa ‘Cheusi’ na Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kumrushia live kidigitali, Mkuu wao aliyekuwa Makao Makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam.
Shamsa Ford akipozi.
Mkuu akiwa ofisini kama kawaida anaangalia saa yake ya mkononi na kubaini kuwa ni zaidi ya saa 3 usiku hivyo anamtwangia kijana wake, Musa Mateja ‘Toz’ aliyempanga kwenye onesho la Machozi Bendi, Ukumbi wa Nyumbani Lounge, Namanga jijini Dar.
Saa 3:12 usiku
SHAMSA FORD ANASWA AKIKATIKA
Makao Makuu: Mateja najua upo kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge hapo Namanga kama nilivyokupanga unafuatilia kwa makini  shoo ya Lady Jaydee, sijui unaweza kuniambia sasa vituko vinavyoendelea hapo?
Mateja: Yeah, hujakosea kiongozi wangu maana ni kweli nipo hapo na sasa Lady Jaydee yupo jukwaani anaporomosha burudani.
Makao Makuu: Oke, vipi suala zima la watu wapo wa kutosha maana hali ya hewa ya mvua wengi wamesimama kwenda viwanja.
Mateja:Kiukweli watu wapo wa kutosha maana shoo inafanyikia ndani na kwamba kuna usalama wa kutosha hata kama mvua itanyesha kubwa kiasi gani?
Makao Makuu: Kuna mastaa gani hapo?
Mateja:Karibu yangu namuona Shamsa Ford tena kapendeza ileile na anazungusha nyonga kwelikweli nahisi ameshapiga maji ya zamzam maana kila mtu anamkodolea macho utafikri yuko kwenye mashindano. Yaani bahati yake yupo na bwanaa’ke angekuwa peke yake wajanja wenye hela zao wangemnasa.
Makao Makuu: Sawa Mateja piga kazi ngoja nimcheki, Dustan Shekidele ‘Mzee wa Mji Kasoro Bahari’.
Saa 4:56 usiku
MACHANGUDOA WAFILISI MSINGI WA MUUZA KUKU
Shekidele: Naam Mkuu wangu nakupata sawia.
Makao Makuu: Haya niambie uko wapi na nini kinaendelea?
Shekidele: Mkuu nilikuwa ndani ya Ukumbi wa Makuti hapa Msamvu kwenye onesho la Kundi la Jahazi Modern Taarab lakini nikatonywa umbeya.
Makao Makuu: Umbeya upi huo?
Shekidele: Hapa nilipo ukivuka barabara kuna eneo maarufu la machangu karibu na gesti ya Itigi kuna mfanyabishara wa kuku kutoka Singida aliingia gesti na changu lakini katika mazingira ya kutatanisha changu alipoondoka jamaa akajikuta laki nane zake zilizokuwa kwenye waleti yake hazipo.
Makao Makuu: Duh, sasa kafanyaje?
Shekidele: Mkuu hapa ni kilio tu, jamaa analia kama mtoto anasema kuku wenyewe aliwachukua kwa mali kauli huko kwao Singida hivyo hajui atasemaje.
Makao Makuu: Kiranga kimemponza huyo acha aingizwe mjini, ngoja niwasiliane na Shakoor Jongo ‘Zungu Fedha’.
Saa 6:18 usiku
MLEGEZO WAMPORONYOKA BLAZAMENI MBELE YA WAKWE
Shakoor: Naam Mkuu wangu habari za Ijumaa Kuu?
Makao Makuu: Salama kijana, hebu niambie uko pande zipi?
Shakoor: Mkuu niko ndani ya Ukumbi wa Escape One hapa Mikocheni yaani hapa ni kama mamtoni kuna nyomi la vijana linakula ujana.
Makao Makuu: Dah, huo ukumbi naupendaga sana yaani upo ufukweni kabisa, vipi kuna vituko gani hapo?
Shakoor: Mkuu kuna familia imekuja kula ujana hapa sasa kuna brazameni alivaa suruali mlegezo kwa bahati mbaya wakati akijishaua kutembea kwa miondoko ya kisharobaro bega moja juu lingine chini huku akikanyaga hatua kama mguu mmoja mbovu mlegezo wake umemporonyoka tena mbele ya shemeji zake na wazazi wa mchumbaa’ke.
Makao Makuu: Ayaa duh, aibu sana lakini akome kuvaa milegezo. Ukipata mpenyo mpige picha, ngoja nimsake Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos.
Saa 7:15 usiku
Bukos: Naam Mkuu nakupata sawia, kama ulivyonipanga niko hapa Ukumbi wa Cheetoz.
Makao Makuu: Nini kinaendelea hapo?
Bukos: Mkuu Bendi ya Mashujaa Musica ‘Watoto wa Mamaa Sakina’ wanafanya makamuzi.
Makao Makuu: Umeona kituko gani hapo?
Bukos: Nimemshuhudia dada mmoja ananyonyana juisi na wanaume karibu watano kwa nyakati tofauti, hivi tunavyoongea amebanwa kwenye kona yenye mwanga hafifu na mwanamuziki wa hii bendi, Raja Raza nahisi naye anataka kumpa juisi.
Makao Makuu: Mmh huyo labda anasambaza virusi vinavyosababisha homa ya ini, achana naye ngoja nimsake, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’.

Saa 8:29 usiku
MZUNGU AMMWAGIA DOLA BANANA
Makao Makuu: Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ nafikiri uko pande za Club East 24 kwenye onesho la B Band, hebu nijuze umeshanasa vituko gani hapo?
Mnally: Mkuu kuna kali moja ya mwaka imetokea hapa.
Makao Makuu: Enhee, endelea Mnally nakusikia…
Mnally: Kuna Mzungu mmoja mrefu sana anammwagia Madola Banana kisa, kamkuna na kibao kinachoitwa London Beats kilichopigwa na Kenn Thomas, huyu mtasha anasema kinamkumbusha familia yake iliyopo kwao (Uingereza).
Makao Makuu: Sawa Mnally piga kazi, ngoja nimsake Haruni Sanchawa ambaye yuko doria maeneo ya Ukonga.

Saa 8: 56 usiku
VIJANA WA KOVA WAIMARISHA ULINZI KILA KONA
Sanchawa: Naam Mkuu wangu nakupata, kama ulivyonipanga nimepita maeneo ya Gereza la Ukonga, FFU na sasa niko kwenye bwalo la maofisa wa magereza, kwa kweli huko hali ni shwari, vijana wa Kamanda Kova wameimarisha ulinzi kama kawaida yao hasa kwa nyakati kama hizi za sikukuu.
Makao Makuu: Vipi kuna vituko ulivyoviona?
Sanchawa: Mkuu kweli mapenzi yana nguvu, hivi tunavyoongea nipo maeneo ya bwalo la maofisa wa magereza, namuona afisa mmoja wa FFU amepigwa makofi kama matatu na kisichana, hivi tunavyoongea huyu afisa amekalishwa kwenye kiti na haka kasichana eti hakamruhusu kwenda popote kisa wivu. Huyo mheshimiwa nasikia kaoza kabisa kwa haka kabinti ndiyo maana kanamtesa.
Makao Makuu: Aah huo uzoba sasa kupenda gani huko? FFU wanavyoogopeka halafu yeye afisa mzima anakuwa zoba. Najua hapo kupiga picha haiwezekani we chukua data tu ukimaliza wapigie wenzako uwaambie mkapumzike.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger