Tuesday, 22 April 2014

Picha:HII NDIO HATI YA MUUNGANO

...
hatiMiongoni mwa ishu kubwa ambazo zimeendelea kuchukua headlines kwenye bunge la katiba ni hii ya hati ya Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ambapo baadhi ya wajumbe wanaounga mkono uwepo wa serikali tatu wamesema hati hiyo haipo hata kwenye umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefuye ameamplify taarifa hizi huku akionyesha hati hiyo ya muungano Ikulu leo April 14 2014 Dar es salaam akianza kwa kusema >>‘siku 12 zijazo tutakua tukisherehekea sikukuu ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’
‘Inasikitisha sana kuwa leo miaka 50 baadae ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna hati ya Muungano,waasisi wa taifa letu ambalo tarehe 22 April 1964 kule Zanzibar walitia saini hati hiyo mbele ya mashuhuda nao wameonekana kama walichokifanya kilikua ni kiini macho’
‘Kwa hiyo waliongoza taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hiko kwa miaka yote hadi mwenyezi Mungu alipowachukua,mambo yote mawili yametusononesha sana wananchi wanaoipenda nchi yao wanaoipenda waasisi wa nchi yao na wanaouenzi Muungano wetu’
‘Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo na ilikuwepo siku zote hata hivyo lazima tukubaliane kuwa zipo hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu kama taifa huru,kama jamhuri huru,kama muungano huru ambazo tunazihifadhi kama mboni ya jicho’
‘Hati hizo ni pamoja na hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961,hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962 na hatimaye hati ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964,hati za namna hii zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala kuharibika,kwa kawaida hatuzitoi tunazifungia ili kuzihifadhi’.
72ikulu
63ikulu
69ikulu
46ikulu
53ikulu
68ikulu
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger