Dondoo muhimu za nilichoongea Leo Bungeni
1.
Hivi sasa Serikali ya 3 imejificha, ipo. Gharama ni zile zile. Sio
lazima tuwe na Marais 3, hatujengi ikulu Mpya. Gharama za Wizara za
Muungano zipo ndani ya Bajeti ya sasa ya Serikali mbili. Hakuna taasisi
Mpya zaidi ya Tume za uwajibikaji nk.
2.
Hatuhitaji kuongeza kodi, tunahitaji kuondoa ubadhirifu na kudhibiti
matumizi yasiyo ya lazima. Tunapoteza Mapato lukuki kwenye misamaha ya
kodi (theluthi ya mapato ya idara ya forodha inasamehewa,
sawa na tshs 2 trilioni kwa mwaka), ukwepaji wa kodi (asilimia 5 ya
Pato la Taifa inapotea, sawa na tshs 2.3 trilioni kwa mwaka ) na
ubadhirifu mwingine uliokithiri. Hivyo udhibiti wa asilimia 50 tu wa
misamaha ya kodi na ukwepaji kodi unaongeza mapato zaidi ya trilioni 2
ambazo Serikali ya Muungano inaweza kugawa kwa Washirika kwa miradi
maalumu ya kitaifa.
3.
Serikali 3 zitaweka Uwazi wa Mapato na zitaweka Uwajibikaji kwa
serikali kutazamana zenyewe. Hizi za sasa zimejaa lawama sababu hakuna
Uwazi. Naomba kuuliza, fedha za mapato kutoka TCRA lini zimeenda
Zanzibar? Mawasiliano ni jambo la Muungano. Lini fedha za TCAA zimeenda
Zanzibar? Gesi Asilia ni jambo la Muungano, hivi Zanzibar wanapata mgawo
wa asilimia ngapi kutoka gesi ya Songosongo? Anga ni jambo la Muungano,
fedha za chenji ya rada zimerudi, Zanzibar imepata kitabu hata kimoja?
Mimi ni mwenyekiti wa PAC, najua haya ninayosema na hamtayamaliza katika
S2 sababu ya confusion ya Muundo. Tatu ni Muundo unaoeleweka. Tukiamua
zifanye kazi zitafanya.
0 comments:
Post a Comment