Friday 18 April 2014

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA TOKA VYAMA VYA UPINZANI JANA JIONI WALIGOMA NA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.....HIZI NI PICHA ZA TUKIO HILO

...


Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao



Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao
***********

Wajumbe karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza.
 
Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
 
Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko.
 
Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu kubwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger