WAZIRI
wa Fedha, Dk Phillip Mpango, amemtaka Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almas
Maige (CCM) kumpa ushahidi ikiwemo majina ya wafanyakazi wa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), aliowatuhumu kufanya biashara na mwajiri wao.
Dk
Mpango alisema hayo Jumatano usiku alipokuwa akijibu hoja za wabunge
kuhusu Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango na kuongeza kuwa akipewa
ushahidi huo, ataufanyia kazi.
Awali
katika mchango wake, Maige alisema anao ushahidi wa maandishi (huku
akiwa ameushika), unaoonesha kuwa kati ya mashirika ya umma yanayovunja
Sheria ya Manunuzi, BoT ipo.
Alidai
kuwa Sheria ya Manunuzi imetoa fursa ya kuanzishwa kwa vitengo na idara
za manunuzi (PMU), lakini fursa hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na vijana
wa vitengo, hivyo kuiibia Serikali.
Kwa
mujibu wa madai ya Maige, katika benki hiyo kuna vijana wamefungua
makampuni ambao wamekuwa wakiyatumia kuomba zabuni za benki hiyo na
kuyalipa.
Mbali
na tuhuma hiyo, Maige ambaye alitangaza maslahi kuwa yeye ni mkandarasi
wa daraja la kwanza, alidai pia kuna vijana wengine wamekuwa wakitoa
zabuni kwa kampuni za nje ya nchi, ili watumie zabuni hiyo kupata safari
za nje.
Alidai
kuwa vijana hao baada ya kutoa zabuni kwa kampuni za nje, hutengeneza
safari za kwenda kufanya uhakiki (due diligence) katika nchi zinakotoka
kampuni hizo, ambako huko hupokea rushwa.
Katika
kuthibitisha hilo, Maige alidai kuwa vijana hao wamediriki kutoa zabuni
kwa kampuni iliyofungiwa na Mamlaka ya Manunuzi ya Umma Tanzania
(PPRA).
Akijibu
hoja hiyo, Dk Mpango alisema tuhuma hizo ndio kazisikia bungeni, hivyo
hana uhakika ila akipewa ushahidi ataufanyia kazi kwa kuwa, utumbuaji
majipu umesaidia kuongeza mapato na kutoka mfano wa makusanyo ya Sh
trilioni moja kila mwezi.
Hivi
karibuni, Serikali ilisitisha utoaji wa Sh bilioni 925 zilizokuwa
zimeidhishwa na BoT kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni ya
Serikali.
Mbali
na hilo, Serikali iliagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali
kilikuwa chini ya BoT na baadaye kupelekwa wizarani, kirejeshwe mara
moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.
Kabla
ya agizo hilo, ilielezwa kuwa malipo hayo yalikuwa yameidhinishwa na
BoT kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni mbalimbali lakini Serikali
ikaagiza fedha hizo zirejeshwe Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya
kufanyiwa uhakiki upya.
0 comments:
Post a Comment